[Latest Updates]: Wachimbaji madini Namungo waomba vifaa

Tarehe : Dec. 17, 2018, 10:08 a.m.
left

Na Greyson Mwase, Ruangwa

Wananchi katika kijiji cha Namungo kilichopo Wilayani Ruangwa mkoani Lindi wameiomba Serikali kupitia Wizara ya Madini kuwapatia vifaa bora ili kuboresha  uchimbaji wa madini na kuchangia kwenye pato la taifa kupitia Sekta ya Madini.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kushoto) akifafanua jambo alipofanya ziara katika Mgodi wa Dhahabu wa Namungo uliopo Wilayani Ruangwa mkoani Lindi ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku mbili katika mkoa huo yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini pamoja na kutatua kero mbalimbali. Katikati ni Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Lindi, Sophia Omari.[/caption]

Wameyasema hayo leo  tarehe 14 Desemba, 2018 katika mkutano wa hadhara uliofanywa katika kijiji hicho ikiwa ni sehemu ya  ziara ya siku mbili ya  Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo mkoani Lindi yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini pamoja na kutatua kero mbalimbali.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wenzake, Dickson Baltazary ambaye ni mchimbaji mdogo wa madini ya dhahabu alisema kuwa, wamekuwa wakichimba madini kwa kutumia zana duni hali inayowasababishia kushindwa kufikia malengo yao kwenye uzalishaji.

Baltazary aliongeza kuwa, iwapo watapata fedha kupitia mikopo na ruzuku Serikalini kupitia Wizara ya Madini wataweza kufanya shughuli zao za uchimbaji wa madini kwa ufanisi na kuchangia zaidi kwenye mapato ya Serikali.

Akizungumza na wachimbaji hao mara baada ya kupokea kero mbalimbali, Naibu Waziri Nyongo alisema kuwa, Serikali imeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa Sekta ya Madini inakuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi kupitia wachimbaji wadogo ambapo mpaka sasa maeneo yameanza kutengwa kwa ajili ya uchimbaji madini.

Aliendelea kusema kuwa Serikali inaangalia utaratibu mzuri utakaowawezesha kupata ruzuku.

Wakati huohuo, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nangurugai Wilayani Ruangwa mkoani Lindi Naibu Waziri Nyongo aliwataka wananchi kuunga mkono uwekezaji wa uchimbaji wa madini ya kinywe (graphite) unaotarajiwa kufanya na kampuni ya utafiti wa madini hayo ya Chilalo Graphite Mine.

Aidha, aliwapongeza wananchi hao kwa kuunga mkono uwekezaji huo kwa kuwa na subira wakati wa tathmini iliyofanywa miaka miwili iliyopita na kuitaka kampuni ya Chilolo kurudia tathmini kwani thamani ya mali imebadilika.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kulia) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nangurugai kilichopo Wilayani Ruangwa mkoani Lindi.[/caption]

Akielezea manufaa ya mradi huo, Nyongo alieleza kuwa ni pamoja na ajira 480 kutolewa wakati wa ujenzi wa mgodi na ajira 250 kutolewa mara baada ya uendeshaji wa mgodi kuanza.

Alieleza manufaa mengine kuwa ni pamoja na kukua kwa uchumi wa Wilaya ya Ruangwa kutokana na ongezeko la mapato yatokanayo na uzalishaji wa madini hayo.

“Madini ya kinywe yana soko kubwa duniani  kutokana na kampuni nyingi kutumia madini hayo katika utengenezaji wa betri za magari, ni vyema mkachangamkia fursa mbalimbali zitakazojitokeza wakati wa utekelezaji wa mradi,” alifafanua Nyongo.

Katika hatua nyingine, Nyongo aliutaka mgodi huo kuhakikisha unatoa ajira kwa wananchi wenye sifa wanaozunguka karibu na mgodi kabla ya kufikiria kuajiri wageni kutoka katika mikoa mingine.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals