[Latest Updates]: Dkt. Mpango atoa Maagizo Sita Akifungua Mkutano wa Nne wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini Mwaka 2022 tarehe 22 Februari, 2022

Tarehe : Feb. 22, 2022, 11:17 a.m.
left

Sekta ya Madini ni moja ya Sekta ya kipaumbele na Mhe. Rais anafuatilia sana mijadala na mapendekezo yanayotolewa kupitia mikutano hii, Serikali iko tayari kushirikiana na wawekezaji wa ndani na nje.

Mikutano hii inasaidia kupokea maoni, michango na hivyo kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara ya madini.

Maagizo

Wawekezaji katika miradi ya ubia na Serikali tunawasisitiza mharakishe utekelezaji wa makubaliano ili watanzania waweze kunufaika na fursa zitakazotokana na uwekezaji husika.

Ni dhahiri kwamba, wachimbaji wa madini kwa kiwango chochote unaenda sambamba  na uharibifu wa mazingira. Hivyo nawakumbusha wachimbaji wote wakubwa na wadogo kuzingatia Sheria za usimamizi wa mazingira.

Wawekezaji wote mnaowajibu wa kuhakikisha kuwa shughuli zenu za uchimbaji, uchenjuaji na uchakataji wa madini zinatekelezwa kwa mujibu wa Sheris na taratibu ili tuweze kunufaika na madini yetu sambamba na nyinyi kupata faida

Wawekezaji wote na hususan wawekezaji wakubwa tunawataka wazingatie matakwa  yanayotokana na tathmini ya athari kwa mazingira na jamii na kuzingatia misingi ya uzalishaji endelevu, matumizi ya mbinu bora za uzalishaji na teknolojia rafikikwa mazingira.

Serikali inawaasa wawekezaji pamoja na wachimbaji kutojihusisha na ajira za watoto na badala yake muongeze juhudi hususan katika  kuhamasisha , kukuza uelewa na kujenga uwezo wa jamii na wachimbaji wadogo na hususan wanawake kwa kupitia  wataalamu wenu wa teknlojia.

Tunazikumbusha kampuni zote zinazowekeza katika sekta hii zihakikishe zinatekeleza ipasavyo takwa la Kisheria la kuandaa mipango ya ufungaji migodi na kuweka hati fungani ya urekebishaji wa mazingira.

Tunawasihi benki na Taasisi za Fedha kushirikiana na Shirika letu la Madini la taifa (STAMICO) kubuni  namna bora zaidi ya kuwawezesha  wachimbaji wetu wadogo wakati Serikali inalifanyia kazi suala la kuanzisha benki maalum ya madini.

Wizara iwasilishe kwa mamlaka taarifa ya mapendekezo ya mkutano huu.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals