Imeandaliwa na:
Asteria Muhozya, Simanjiro
Afisa Habari,
Wizara ya Madini,
Kikuyu Avenue,
P.O Box 422,
40474 Dodoma,
Simu: +255-22-2121606/7, Nukushi: +255-22-2121606,
BaruaPepe: info@madini.go.tz,
Tovuti: madini.go.tz
Tarehe : Aug. 3, 2018, 5:55 a.m.
erikali imesema inajiandaa kuja na mbinu za kisasa zaidi za ukaguzi na ulinzi katika ukuta unaozunguka migodi ya Tanzanite, Mirerani ili kudhibiti utoroshaji wa madini hayo yanayopatikana Wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara.
Waziri wa Madini Angellah Kairuki akisisitiza jambo wakati akizungumza na katika mkutano wa hadhara na wananchi wanaofanya shughuli zao ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya tanzanite, mirerani. Wanaofuatilia mbele ni Mbunge wa Simanjiro James Ole Milya (kulia) na kushoto ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Tumain Magesa.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Madini Angellah Kairuki tarehe 2 Agosti, 2018 wakati wa mkutano wa hadhara ulishirikisha wamiliki wa migodi, wachimbaji, wauzaji na wote wanaofanya shughuli zao za ndani ya ukuta huo.
Alisema, mabadiliko ya ujenzi wa ukuta huo ni chanya ambayo yamelenga kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta ya madini ili kuongeza mchango wa sekta husika katika pato la taifa.
Waziri Kairuki alieleza ili shughuli za uuzaji na ununuzi ziweze kufanyika ndani ya eneo hilo, tayari Serikali imejenga sehemu maalum kwa ajili ya shughuli hizo na kuongeza, “ baada ya kukamilika jengo hilo kutakuwa na sehemu kwa ajili ya Broker kufanyia shughuli zao hapo hapo ndani ya ukuta.”
Aliongeza, tayari Mkataba wa ujenzi wa Kituo cha kufanyia shughuli zote zinazohusu biashara ya madini ya tanzanite kwa ujumla (One Stop Center) umekwishakabidhiwa na ndani ya muda mfupi ujao, ujenzi wa jengo husika utaanza.
Sehemu ya wananchi waliofika katika mkutano wa hadhara ambao ulijumuisha wamiliki wa migodi, wachimbaji, wauzaji, wanunuzi na wanaofanya shughuli mmbalimbali ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya tanzanite, Mireran wakimsikiliza Waziri wa Madini Angellah Kairuki, hayupo pichani
Akitoa ufafanuzi kuhusu taratibu za kuingia na kufanya shughuli za uchimbaji ndani ya ukuta, Waziri Kairuki alisema taratibu za ukaguzi zinalenga katika kudhibiti utoroshaji madini na hivyo kuwataka wadau wote kutoa ushirikiano wakati wa zoezi la ukaguzi katika ukuta huo na kuongeza kuwa, aina ya ukaguzi unaofanywa kwa sasa ni wa muda mpaka hapo taratibu maalum za ukaguzi zitakapokuwa tayari.
Akitoa ufafanuzi kuhusu wazawa wenye leseni za uuzaji kulipa ada kwa kutumia Dola za Marekani, Waziri Kairuki alieleza kuwa, kwa kuwa Kanuni za eneo la Mirerani zimeandaliwa na Waziri mwenye dhamana na sekta, suala hilo litafanyiwa kazi ili kipengele husika kiweze kufanyiwa marekebisho na hivyo kuwawezesha kulipia kwa fedha za Tanzania. Pia, aliongeza kuwa, katika kipindi hiki ambacho mabadiliko hayo hayajafanyika, wahusika watalazimika kuendelea na utaratibu uliopo.
Ili kuongeza kasi ya shughuli ya uthamini wa madini hayo, waziri Kairuki alisema wizara yake itaongeza idadi ya wataalam kutoka mmoja hadi wanne ili kuongeza kasi ya kufanya shughuli husika.
Pia, Waziri Kairuki aliwataka wamiliki wa migodi kuhakikisha wanakuwa na mikataba ya wafanyakazi katika migodi yao na kuongeza kuwa, suala la maslahi ya watumishi ni jambo ambalo linapaswa kupewa kipaumbele na wadau wote katika sekta husika.
Sehemu ya wananchi waliofika katika mkutano wa hadhara ambao ulijumuisha wamiliki wa migodi, wachimbaji, wauzaji, wanunuzi na wanaofanya shughuli mmbalimbali ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya tanzanite, Mireran wakimsikiliza Waziri wa Madini Angellah Kairuki, hayupo pichani
“Maslahi ya wafanyakazi yanatakiwa kuwa namba moja. Mimi ni Mbunge niliyechaguliwa kupitia umoja wa vyama vya wafanyakazi hivyo suala la maslahi ya wafanyakazi lazima nilisimamie kikamilifu,” alisisitiza Kairuki.
Akizungumzia suala la usafiri ndani ya ukuta, alisema zoezi husika litaendelea kama ilivyo sasa na kutumia fursa hiyo kukaribisha wawekezaji zaidi katika huduma ya kutoa huduma ya usafiri ndani ya ukuta huo.
Pia, alitumia fursa hiyo kuwataka wadau wote katika eneo hilo kuwa waaminifu na kushirikiana na serikali na hususan ofisi ya Madini katika kutoa taarifa za utoroshaji madini hayo.
Mwisho aliwataka Maafisa Madini kuendelea kutoa elimu ya Sheria ya Madini pamoja na taratibu zake pia, Mbunge wa eneo husika aendelee kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuwepo kwa ukuta huo ili kuwawezesha wadau wote kuwa na uelewa wa pamoja.
Kwa upande wake, Mbunge wa Simanjiro James Ole Milya, alisema alimweleza Waziri Kairuki kuwa kero kubwa katika eneo husika ni baina ya wamiliki wa migodi na wafanyakazi na hivyo kumtaka Waziri kuona namna ya kushughulikia suala hilo.
Pia, alipendekeza kuundwa kwa kamati mbili moja ikiwa ya wamiliki na wafanyakazi kwa lengo la kuondoa mvutano uliopo sasa kati ya pande mbili.
Imeandaliwa na:
Asteria Muhozya, Simanjiro
Afisa Habari,
Wizara ya Madini,
Kikuyu Avenue,
P.O Box 422,
40474 Dodoma,
Simu: +255-22-2121606/7, Nukushi: +255-22-2121606,
BaruaPepe: info@madini.go.tz,
Tovuti: madini.go.tz
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.