[Latest Updates]: Serikali na Wizara ya Madini kusaini Mkataba wa Utendaji kazi

Tarehe : Dec. 2, 2019, 8:18 a.m.
left

Na Issa Mtuwa - Dodoma

Mafunzo ya  Mkataba wa Utendaji Kazi kwa Serikali na Taasisi za umma yameanza kufanyika kwa viongozi waandamizi wa wizara ya Madini, wakuu wa idara na vitengo na maafisa bajeti wa kila idara na kitengo kuhudhuria mafunzo hayo yanayotolewa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara ya madini jijini Dodoma kuanzia leo tarehe 2 Desemba 2019.

Mafunzo hayo yanayotolewa kwa wizara zote na tasisi za umma kwa awamu yanalenga kuziwezesha Taasisi za Serikali kuandaa na kutekeleza mikataba ya utendaji kazi serikalini tofauti na ule mkataba wa upimaji wa utekelezaji majukumu kwa watumishi wa umma (OPRAS)

“Mikataba hii ni kwa mujibu wa Waraka Na. 1 wa Mkuu wa Utumishi wa Umma wa mwaka 2018, pamoja na mambo mengine unatoa maelekezo kwa wizara, idara  zinazojitegemea, taasisi, mamlaka, sekretarieti za mikoa, mamlaka za serikali za mitaa, wakala wa serikali na mashirika ya umma kuandaa na nakufanya utekelezaji wa mikataba ya utendeji kazi kwa kufuata malengo, shabaha na viashiria vitakavyo ainishwa mwazo wa mwaka” alisema Charles Nakembetwa Afisa  Takwimu Mkuu ambae ni mwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Pamoja na mambo mengine aliyobainisha kuhusu mkataba huo wa utendaji kazi, serikali na taasisi za umma zitakuwa zinapimwa kwa vigenzo mbalimbali vya utendaji na kwamba upimwaji huo utashindanishwa  wizara  kwa wizara, taasisi kwa taasisi, mikoa kwa mikoa, mashirka kwa mishirika  n.k na kupata mshindi wa utendaji kazi kwa mwaka husika kwa kila kundi.

“Kutakuwa na siku maalum ya utoaji tuzo (zawadi) kwa watakao tekeleza mkataba wa utendaji kazi vizuri kwa kila kundi na kwamba kwa watakaoshindwa kutekeleza mkataba huo pia watapewa muda kujirekebisha na baadhi kupewa adhabu kwa mujibu wa vigezo vitakavyo ainishwa” Alisema Kamugisha Rufulenge ambae ni mwenzeshaji mwenza.

Ameongeza kuwa kwa mujibu wa mkataba huo, katika ngazi ya wizara mtendaji mkuu wa usimamizi wa utayarishaji na usimamizi wa utekelezaji wake atakuwa Mkurugenzi wa Sera na Mipango (DPP) atakae simamia masuala yote kuhusu mkataba huo.

Akiongea mara baada siku ya kwanza ya  mafunzo hayo, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Edwini Igenge amesema mafunzo hayo yanaongeza hamasa kwa watendaji kuongeza bidii katika utendaji kazi na kwamba kwa upande wa Wizara ya Madini wako teyari kwa ajili ya uandaji na utekelezaji wa mkataba huo wa utendaji kazi.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Madini Issa Nchasi amesema serikali imefanya kazi kubwa kuboresha utumishi wa Umma na mifumo mbalimbali ambayo inarahisisha utendaji kazi akitolea mfano mfumo wa malipo ya mishahara ya wafanyakazi (Payroll control).

Washiriki wa mafunzo hayo hawakukosa kujadili kuhusu masuala ya mishahara ya watumishi wakijadili katika sura tofauti tofauti hoja zikielekezwa kwa wawezeshaji huku mengine yakitolewa ufafanuzi mengine wawezeshaji wakiahidi kuyachukuwa na kuyapeleka mbele kwa hatua zaidi.

Mhsabu  Mkuu wa Wizara ya Madini Anthony Tarimo alitaka kufahamu kuna hatuagani iliyofikiwa katika kufanya harmonization ya mishahara kwa watumishi wa kada zote kama ambavyo iliwahi jadiliwa kwa nyakati tofauti tofauti huku Mkurugenzi Msaidizi  wa Rasilimali Watu Kabigi Nsajigwa akizungumzia mitazamo na mijadala inayozungumzia kuhusu upunguzwaji wa mishahara hasa kwa watumishi wa mashirika, taasisi, mamlaka n.k. Amesema kimsingi kuna haja ya kutazamwa mtanzamo huo kama ambavyo fikra za wengi wakitaka wenye mishahara mikubwa wapunguziwe Ameongeza kuwa kitendo cha kuwapunguzia mishahara watu inaweza kuleta ufanisi hafifu kwani maamuzi hayo yanapaswa kuzingatia mambo mengi kabla ya uwamuzi huo huku akitolea mfano hapo nyuma ilivyowahi kupunguza mishahara kwa watumishi wa kada ya uhasibu kwenye  baadhi ya maeneo.

Mafunzo hayo ya siku tano yaliyoanza leo yamehudhuriwa viongozi waandamizi wa WIzara ya Madini akiwemo Kaimu Katibu Mkuu Edwini Igenge, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Issa Nchasi, Mkurugenzi wa Sera na Mipango Augustine Olal, Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Ndani Mathias Abisai, Mwasibu Mkuu Anthony Tarimo, Kaimu Mkurugenzi wa Manunuzi Ashura Urassa na Wakuu wote wa Idara na Vitengo, Wakurugenzi Wasaidizi, Makamishna Wasaidizi na Maafisa Bajeti wa kila idara na vitengo.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals