[Latest News]: Waziri Biteko Atoa Siku Saba kwa Wachimbaji Kulipa Madeni ya Wananchi Wilayani Bahi

Tarehe : July 4, 2022, 1:05 a.m.
left

Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko, ametoa wiki moja kwa wachimbaji wa madini ya Chuma wilayani Bahi Mkoa wa Dodoma kulipa madeni wanayodaiwa na wananchi katika migodi hiyo wanaofanya kazi ya kuponda za madini hayo.

Agizo hilo amelitoa Julai 4, 2022 wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Asanje mara baada ya kutembelea maeneo ya wachimbaji wa chuma na kupokea malalamiko.

Dkt.Biteko, amemwelekeza Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma kusimamia agizo hilo kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda ili wanachi hao wa Asanje walipwe fedha zao wanazowadai wawekezaji hao.

"Mhe  Mkuu wa wilaya, kama kuna mtu atakuwa hajalipwa hadi jumatatu Afisa Madini unasimamisha mgodi huo mara moja bila masharti yoyote, uandike kabisa kwa maelekekeao ya Waziri nasimamisha," amesisitiza.

Aidha, amewataka wachimbaji wa madini na wawekezaji katika Sekta ya Madini kuhakikisha wanashirikisha wananchi katika mipango yao ya uwekezaji kabla hawajawekeza kwenye miradi hiyo ili kupunguza malalamiko yanayojitokeza mara kwa mara. Amesema, ushirishwaji utasaidia kujua vipaumbele vya wanachi ili iwe rahisi kwa utekelezaji.

"Nataka niwaambieni wenye leseni, leseni hizi mmepewa kwa niaba ya Watanzania wengine. Kwa kuwa tumewapa wenzetu leseni ya kuchimba matarajio ya Serikali ni kwamba hawawezi kugeuka tena kuwa kero kwa watu ambao wako maeneo ya kuchimba,"amesema.

Naye, Mbunge wa Jimbo la Bahi, Kenneth Nolo amesema, ziara ya Dkt.Biteko katika Kijiji cha Asanje kusikiliza malalamiko ya wanachi hao, imekuwa na manufaa kwa wananchi na matarajio makubwa katika shughuli za uchimbaji madini.

Katika ziara hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Munkunda amemshukuru Dkt.Biteko kwa kuweza kufika na kusikiliza changamoto za wananchi hao kwani ilikuwa ni kiu kubwa ya kuweza kufikisha malalamiko yao kwake.Wilaya ya Bahi yanapatikana madini mbalimbali yakiwemo dhahabu, chuma na madini ujenzi.

ReplyForward

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals