[Latest Updates]: Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Madini Watembelea Kituo cha TGC

Tarehe : March 23, 2025, 2:21 a.m.
left

 Arusha

Wajumbe wa Baraza la  Wafanyakazi Wizara ya Madini, Machi 22, 2025, walitembelea Kituo cha Jemolojia Tanzania ( TGC) kilichopo jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya Wajumbe hao kujifunza kuhusu shughuli zinazotekelezwa na Kituo hicho.

Katika ziara hiyo, pia walitembelea eneo la mradi wa ujenzi wa Jengo la ghrorofa Nane linalotarajiwa katika Kituo hicho  pamoja na kutembelea maeneo mbalimbali ya shughuli za utoaji mafunzo ya uongezaji thamani madini ya vito na miamba yanayotolewa na Kituo hicho.

Akizungumza katika ziara hiyo, Kaimu Mratibu Wa Kituo hicho Ally Maganga alisema kwa sasa Kituo hicho kina jumla ya wanafunzi 110 wanaosoma masomo ya muda mrefu  na Sita wanachukua mafunzo ya muda mfupi.

"Tumepiga hatua kwenye uzalishaji wa mapambo kutokana na  kupata vifaa  vya  teknolojia ya juu na ni imani yangu baada ya kukamilika kwa mradi huu Kituo hiki kitapiga hatua zaidi," alisema Maganga.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals