[Latest Updates]: Serikali Yakamilisha Utiaji Saini wa Mikataba ya Ununuzi na Usafishaji wa Dhahabu Nchini

Tarehe : June 17, 2025, 1:18 p.m.
left

Kwa kipindi cha miezi 9 kiasi cha tani 5 za dhahabu safi zanunuliwa.

Lengo ni kununua tani 6 za dhahabu  kwa Mwaka wa 2024/2025.

Viwanda 9 vya kusafisha madini ya metali kujengwa nchini.

Wadau wampongeza Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi kubwa za kuendeleza Sekta ya Madini nchini.

Dodoma

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) itaendelea kuimarisha Mpango wa Ununuzi na Uhifadhi wa madini ya dhahabu yaliyosafishwa kwa kiwango cha asilimia 99.9 kutoka katika migodi na  viwanda vya kusafisha dhahabu ili kuwa na akiba imara ya fedha za kigeni.

Hayo yalisemwa Juni 16, 2025  na Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba  wakati wa utiaji saini wa mikataba ya Ununuzi na Usafishaji wa dhahabu kati ya BoT na kampuni za madini ikiwemo kampuni ya uchimbaji wa Madini ya dhahabu Geita(GGM), Shanta , Backreef na Kiwanda cha Usafishaji dhahabu Geita (GGR).

Dkt. Nchemba alipongeza wizara ya madini na Timu ya Majadiliano kwa kusimamia Mpango huo ambapo mpaka sasa kiasi cha tani 5 za dhahabu safi ya asilimia 99.9 imenunuliwa na kuhifadhiwa (BoT).

Kwa upande wake, Waziri wa Madini Mheshimiwa Anthony Mavunde alisema kuwa, Sekta ya Madini nchini inaendelea kukua kwa kasi mwaka hadi mwaka hii ni kutokana na usimamizi  mzuri , udhibiti wa mianya ya utoroshaji madini  pamoja na mabadiliko ya Sheria na mifumo bora ya Uendeshaji masoko ya madini nchini.

Mavunde alieleza kuwa, katika mwaka wa 2015/2016 Sekta ya Madini iliingiza kiasi cha shilingi bilioni 165 katika Mfuko Mkuu wa Serikali ikiwa ni makusanyo ya mwaka.

Mavunde alibainisha kuwa, kutokana na mageuzi mbalimbali ya kisekta yamepelekea kuongezeka kwa mchango katika Mfuko Mkuu wa Serikali ambapo kwa Mwaka wa 2023/2024 Sekta ya Madini ilichangia shilingi bilioni 753.

Akielezea kuhusu maendeleo kwa mwaka wa 2024/2025, Mavunde ameeleza kuwa mpaka mwezi Juni 2025, Sekta ya Madini imefanikiwa kuchangia shilingi bilioni 970 katika Mfuko Mkuu wa Serikali, ikiwa imebakiza asiimia ndogo kufikia lengo la shilingi trilioni kwa mwaka husika.

Waziri alimshukuru Rais , Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maelekezo yake na  juhudi mbalimbali anazozifanya ili kuhakikisha Sekta ya Madini inaendelea kuwa na mchango mkubwa katika Pato la Taifa.

Naye , Gavana wa Benki ya Tanzania Mheshimiwa Emmanuel  Tutuba aliipongeza wizara ya madini , Tume ya Madini pamoja na Timu ya Majadiliano kwa kuweza kukamilisha taratibu zote za majadiliano na hatimaye kufika muhafaka kwa pande zote.

Tutuba aliongeza kuwa, BoT itaendelea kununua dhahabu kulingana mikataba iliyosainiwa na pande zote kama inavyoelekeza kuhusu ununuzi wa asilimia 20 ya dhahabu inayozalishwa na kusafishwa lengo ni kununua tani 6 kwa mwaka. 

Akifungua hafla hiyo ya utiaji saini , Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali , Mheshimiwa Samweli Maneno alibainisha kuwa, kupitia Sheria ya Fedha kifungu cha 59 kimeipa BoT haki ya kununua dhahabu kwa asilimia 20 ya dhahabu inayozalishwa kubaki nchini.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals