[Latest Updates]: Utafiti wa Uanzishwaji Mgodi Mkubwa wa Dhahabu Waanza Wilaya ya Hanang, Manyara

Tarehe : Nov. 26, 2025, 12:23 p.m.
left

Waziri Mavunde aipongeza Kampuni kwa kukidhi masharti ya Leseni ya Utafiti

Asimamia kwa vitendo lengo la kuongeza eneo la utafiti kutoka 16% hadi 50% ifikapo 2030

Ni utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Rais Samia

Wananchi kunufaika kiuchumi na kijamii mradi ukianza kutekelezwa

 Manyara

Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde (Mb), ametembelea na kushuhudia utekelezaji wa utafiti wa kina wa madini kwa kutumia teknolojia ya ndege nyuki (drone) katika Kata ya Basotu, Wilaya Hanang, mkoani Manyara. Utafiti huo wa jiofizikia unalenga kubainisha maeneo yenye hifadhi ya madini utakaopelekea kuanzishwa kwa mgodi mkubwa wa dhahabu wilayani humo.

Ziara hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa wakati akihutubia Bunge Oktoba 13, 2025 ambapo alitaja utafiti wa madini kama kipaumbele kwa mwaka 2025 - 2030 utakaopelekea kufikia angalau asilimia 50 ya utafiti wa kina wa madini nchini ifikapo mwaka 2030.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Waziri Mavunde amesema utafiti huo ni hatua muhimu kwa maendeleo ya wananchi wa Hanang na Mkoa wa Manyara kwa ujumla, kwani matokeo yake yanatarajiwa kuongeza ajira, kuvutia uwekezaji na kuchochea utekelezaji wa miradi ya kijamii kupitia leseni za uchimbaji madini.

“Tunatarajia utafiti huu utaleta matokeo chanya yatakayobadilisha maisha ya wananchi. Serikali itaendelea kusimamia sekta hii ili iwe chachu ya maendeleo kwa wote,” amesema Mavunde.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Mhe. Almish Hazal, amemshukuru Waziri Mavunde kwa kutembelea eneo la mradi huo na kuendelea kusisitiza umuhimu wa tafiti za madini katika wilaya yake pia, ameiomba Wizara ya Madini kuendeleza kasi hiyo katika maeneo mengine ya Hanang yenye uwezekano wa kuwa na madini.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Cobra Resources Ltd, Bw. Amos Nzungu, amempongeza Waziri Mavunde kwa ushirikiano na uzalendo anaouonesha kwa kufuatilia utekelezaji wa miradi ya utafiti wa madini na kuahidi kukabidhi matokeo ya utafiti mara tu yatakapokamilika.

Kwa upande wa Meneja wa Kampuni ya SkyPM Solution inayofanya utafiti huo, Bw. Paul Madata amesema matumizi ya teknolojia ya ndege nyuki yamerahisisha na kuongeza ufanisi wa utafiti wa awali, kwani inaweza kupima hadi zaidi ya kilomita tatu chini ya uso wa ardhi kwa muda mfupi.

Awali, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Manyara, Mhandisi Godfrey Nyanda ametoa taarifa ya maendeleo ya sekta ya madini mkoani hapo, akibainisha kuwa hadi kufikia robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2025/26 (Julai–Oktoba), wamekusanya asilimia 35.21 ya lengo la makusanyo ya Shilingi Bilioni 2.2 lililopangwa kwa mwaka mzima.

“Tutaendelea kusimamia kikamilifu maagizo ya Mhe. Rais na ya Waziri wetu Mhe. Mavunde ili kuhakikisha sekta ya madini inaendelea kukua na kuimarika hapa Manyara,” amesema Mha. Nyanda.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals