Tarehe : April 11, 2023, 12:21 p.m.
Yaandaa Mpango wa Uhamishaji Makazi Kupisha Mradi wa Dhahabu wa Nyanzaga*
Katibu Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali amefanya kikao jijini Dodoma na Kampuni ya Sotta Mining Corporation Limited (SMCL) inayomiliki mgodi wa Nyanzaga wenye hisa ya asilimia 84 na Serikali ya Tanzania yenye hisa ya asilimia 16.
SMCL inajenga mradi wa dhahabu wa Nyanzaga katika vijiji vya Sotta na Nyabila kata ya Igalula wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza baada ya kupewa leseni ya uchimbaji mkubwa wa madini ya dhahabu mwaka 2021.
Akizungumza katika kikao hicho, Mratibu wa zoezi la uhamishaji makazi wa SMCL Paul Gongi amesema uhitaji wa ardhi kwa ajili ya mradi wa Nyanzaga umepelekea kutengeneza Mpango wa Uhamishaji Makazi na Mpango wa uboreshaji wa maisha.
Pamoja na mambo mengine, Gongi amesema SMCL inajenga mradi wa dhahabu wa Nyanzaga katika vijiji vya Sotta na Nyabila kata ya Igalula wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.
Gongi amesema kusudi la Mpango wa Uhamishaji Makazi ni kutengeneza mfumo wa kina na shirikishi wa Uhamishaji Makazi na kaya zinazoguswa na mradi pamoja na kuhakikisha maisha ya waathirika yanaboreshwa baada ya uhamisho.
Aidha, Gongi amesema eneo la leseni ya mradi wa Nyanzaga lina kilometa za mraba 23.46 na linagusa vitongoji vitano ambavyo ni Sotta A, Nyang'hona, Kadashi, Kaningu B na Nyashimba ambapo linagusa kaya 725 na idadi ya watu 5,690.
Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa SMCL Damian Valente amesema Mtathmini Mkuu wa Serikali amekamialisha zoezi la kutathmini na kinachofuata ni kukamilisha fedha za kulipa fidia kwa walioguswa na mradi huo.
Valente amesema shughuli zote zilizomo ndani ya leseni, miundombinu na makazi yote yatahamishwa kwa sababu ya ukubwa wa ardhi inayohitajika kwa shughuli za uchimbaji, uchenjuaji, uhifadhi mawetaka na miundombinu inayohusika na uchimbaji katika eneo la leseni.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.