[Latest Updates]: Kiwanda cha Kusafisha na Kuongeza Thamani Madini Adimu Kujengwa Ngwala, Songwe

Tarehe : June 4, 2025, 1:41 p.m.
left

Uendelezaji wa Mradi kuanza rasmi    Disemba 2025

Ni mradi wa Madini Adimu utakaogharimu Bilioni 771

Waziri Mavunde azindua zoezi la ulipwaji fidia wananchi 192

Wananchi wamshukuru Rais Samia kwa mazingira ya uwekezaji

Serikali kuvuna mapato ya zaidi ya Trilioni 12 

Ngwala, Songwe

Kampuni ya Mamba Minerals Ltd inayowekeza kwenye mradi wa Madini adimu imeweka wazi mpango wake wa kujenga kiwanda cha kusafisha na kuongeza thamani madini adimu kijijini,Ngwala Mkoani Songwe badala ya kusafirisha madini hayo yakiwa ghafi.

Hayo yamesemwa leo Kijijini Ngwala, Songwe wakati wa uzinduzi wa zoezi la ulipwaji fidia wananchi waguswa wa mradi takribani 192 zoezi ambalo limezunduliwa na Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde.

Akitoa maelezo ya awali, Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mamba Minerals Ltd Ndg. Ismail Diwani amesema zoezi hilo la fidia litagharimu kiasi cha Tsh 5.3 Bilioni kwa kuhusisha wananchi waguswa wa mradi 192 ambapo mpaka sasa wananchi 116 wamepokea malipo yao tayari.

“Hatua hizi ni za awali kuelekea kwenye utekelezaji wa mradi ambapo shughuli rasmi za ujenzi wa mradi zitaanza Disemba 2025 sambamba na ujenzi wa kiwanda cha kusafisha madini adimu na ujenzi wa mtambo wa kufua umeme utakaozalisha megawati 12”Amesema Ismail

Waziri Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Mamba Minerals Ltd kwa ujenzi wa kiwanda cha kusafisha madini hayo hapa nchin ikiwa ni uongezaji wa thamani wa madini hayo kabla ya kusafirishwa ikiwa ni sehemu ya kuitikia wito uliotolewa na Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan juu ya uongezaji thamani madini nchini.

“Mradi huu pamoja na Ajira, mrabaha, ushuru wa Halmashauri pia utaipa serikali mapato ya moja kwa moja ya zaidi ya Tsh 12 Trilioni wakati wote wa uhai wa mgodi.

"Tutahakikisha wananchi wa Ngwala wananufaika na mradi huu mkubwa kupitia maudhui ya ndani (Local Content) na hivyo mradi huu kuwa kichocheo cha maendeleo ya kiuchumi ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Mradi huu una wastani wa mashapo ya Tani 18.5 milioni za madini adimu ni kati ya miradi mikubwa  duniani ya madini adimu na hivyo itaifanya Tanzania kuwa mzalishaji wa malighafi kwa ajili ya vifaa vya matibabu, kieletroniki na ufuaji wa umeme wa upepo," amesema Mavunde.

Naye, Mkuu wa Wilaya wa Songwe Solomon Itunda amesema mradi huo utachochea ukuaji wa sekta ya madini Mkoani Songwe kwa kiwango kikubwa na hivyo kuufanya mkoa huu kuwa kati ya wachangiaji wakubwa katika kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta ya madini.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals