[Latest Updates]: Dkt. Kiruswa Atoa Ushauri Utatuzi wa Mgogoro Uliodumu kwa Miaka 9 Mbogwe

Tarehe : June 6, 2025, 10:46 a.m.
left

Aunda timu ya maridhiano ya wajumbe 17

Asisitiza maridhiano ya kweli ili kumaliza mgogoro baina ya wamiliki wa shamba na wamiliki wa leseni ya madini.

Mbogwe - Geita

Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa ametoa ushauri wa kufanya maridhiano ya kweli  baina ya wamiliki wa mashamba na wamiliki wa leseni ya madini katika machimbo ya dhahabu yaliyopo katika eneo la  Nyakafuru  Wilaya ya  Mbogwe mkoani Geita.

Dkt.Kiruswa ametoa ushauri huo leo tarehe 6 Juni, 2025  katika kikao maalumu kilichowakutanisha pande zote mbili zenye mgogoro na kuwashauri wafanye maridhiano ya kweli  yatakayoleta tija kwa pande zote mbili kwa kuangali haki zilizopo kwa kila upande ambazo ni wamiliki wa mashamba na wamiliki wa leseni.

Katika kuhakikisha maridhiano hayo yanafanikiwa, Dkt.Kiruswa  ameunda timu ya wajumbe kumi na saba watakaoshiriki katika mchakato wote wa kutafuta maridhiano kuanzia ngazi ya kijiji mpaka Mkoa.

Akielezea kuhusu majukumu ya timu hiyo, Dkt. Kiruswa amesema kuwa, lengo la kuunda timu itakayosimamia  maridhiano ni  kuhakikisha haki zinapatikana kwa pande zote mbili hususan katika haki ardhi na haki madini, kufanya tathimini ya gharama husika na kufanya malipo kwa usawa na kuandaa mkataba maalum wa maridhiano utakaosainiwa na kuwasilishwa Wizara ya Madini.

Awali, akielezea kuhusu historia ya mgogoro huo Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Sakina Mohamed amesema kuwa , mgogoro umekuwa wa muda mrefu ambapo mpaka sasa una miaka tisa bila kupata suluhu kwa pande zote, ambapo unapelekea wilaya ya Mbogwe kukosa mapato yanayotokana na uzalishaji wa dhahabu  hivyo amewataka wahusika kutumia fursa iliyotolewa na Dkt. Kiruswa kuhakikisha mgogoro unamalizika kwa wakati.

Pamoja na mambo mengine, Sakina amempongeza Dkt.Kiruswa kwa juhudi mbalimbali anazofanya kuhakikisha mgogoro huo unakwisha kwa kutenda haki kwa pande zote mbili.

Akielezea kuhusu hali ya mgogoro  Afisa Madini Mkazi wilaya ya Mbogwe, Mhandisi Jeremiah Hango ameeleza kuwa, mgogoro huu umekuwa wa muda mrefu Ofisi ya Madini Mbogwe imefanya juhudi mbalimbali za kutatua  mgogoro kuanzia ngazi ya kijiji   mpaka wilaya lakini mpaka sasa muafaka bado haujapatikana.

Kwa mujibu wa Sheria ya Madini Sura ya 123, kifungu cha 95 na 96, kinasema mwenye shamba  ana miliki sehemu ya juu ya ardhi , huku mwenye leseni anamiliki madini yaliyopo  chini ya ardhi katika eneo husika la leseni.

Lakini utaratibu unamtaka mmiliki wa leseni kabla ya kuanza shughuli za uchimbaji atatakiwa kuingia mkataba na mwenye ardhi.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals