[Latest Updates]: Serikali Kuwapatia Mitaji na Mitambo ya Kisasa Wachimbaji Wadogo

Tarehe : Oct. 15, 2023, 8:20 a.m.
left

Singida

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amesema kuwa Serikali imedhamiria kuwasaidia Wachimbaji Wadogo wa Madini katika Mkoa wa Singida kwa kuwapatia mitaji na mitambo ya kisasa ya kuendesha shughuli za uchimbaji. 

Amesema hayo leo Oktoba 15, 2023 wakati akisalimia wananchi eneo la Sagala Wilayani Singida, wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.  Samia Suluhu Hassan mkoani Singida 

Amesema kuwa maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuwasaidia wachimbaji hao kupitia utafiti wa kina wa miamba ili kuwe na taarifa za kutosha zinazohusu maeneo yenye rasilimali madini hapa nchini ili wasifanye shughuli za uchimbaji kwa kubahatisha. 

“Mhe. Rais mkoa wa Singida ni moja ya mikoa iliyojaaliwa na Mwenyezi Mungu kuwa na Rasilimali Madini na hapa kuna wachimbaji wadogo wengi, umeshatupa maelekezo tufanye utafiti wasichimbe tena kwa kubahatisha, lakini vilevile tuwasaidie wapate mitaji na mitambo, Mhe. Rais tuko tayari kufanya hili na tunaanza tarehe 21 mwezi huu pale Dodoma kwa kugawa mitambo hiyo kwa Wachimbaji wadogo wakiwemo hawa Mpipiti na Mtambaa." amesema Mhe. Mavunde. 

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi Oktoba 21, 2023, jijini Dodoma kwenye hafla ya kukabidhi mitambo mitano ya uchorongaji kwa Wachimbaji Wadogo, mitambo hiyo imenunuliwa na Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals