[Latest Updates]: Jukwaa la Nne la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania Katika Sekta ya Madini Lilete Mabadaliko - Ollal

Tarehe : June 18, 2025, 1:35 p.m.
left

MWANZA

Wadau wa madini nchini wametakiwa kutumia Jukwaa la Nne la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta la Madini kama kichocheo cha mabadiliko katika Sekta ya Madini hasa kwenye eneo la ushirikishwaji wa watanzania katika Sekta ya Madini  katika eneo la ajira na utoaji wa huduma kwenye migodi ya madini kama vile  usambazaji wa vifaa na  vyakula.

Hayo yamesemwa jijini Mwanza leo Juni 18, 2025 na Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Madini, Augustine Ollal kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo wakati akifunga Jukwaa la Nne la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta la Madini.

Jukwaa hilo lililoanza mapema Juni 16, 2025 limekutanisha wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na  Wizara ya Madini na Taasisi zake, Taasisi za Serikali, Taasisi Binafsi, Taasisi za Fedha, Kampuni za Uchimbaji wa Madini na Watoa Huduma kwenye Migodi ya Madini.

Amesema kufanyika kwa jukwaa hilo ni mkakati wa Serikali kupitia Wizara ya Madini kuhamasisha ushiriki wa watanzania katika shughuli za uchimbaji, uchenjuaji, biashara ya madini na usambazaji wa bidhaa na huduma kwenye shughuli za uchimbaji wa madini ili wananchi waendelee kunufaika na rasilimali madini na kukuza uchumi wa nchi.

Katika hatua nyingine, amezitaka kampuni za madini kuendelea kutoa kipaumbele kwa watanzania kwenye  ajira na utoaji wa huduma kwenye migodi ya madini.

Wakati huo huo amempongeza Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde kwa kutafsiri maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa vitendo kwenye usimamizi wa Sekta ya Madini hali iliyopelekea mchango wake katika Pato la Taifa kufikia asilimia 10.1.

 Jukwaa hilo lenye kaulimbiu inayosema Ongezeko la Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini ni chachu ya Ukuaji wa Uchumi limeambatana na maonesho yenye lengo la kuelimisha kuhusu fursa za uwekezaji katika Sekta ya Madini.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals