Tarehe : May 24, 2018, 10:55 a.m.
Wizara ya Madini imefanya Semina kwa Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini pamoja na Kamati ndogo ya Sheria ya Bunge juu ya Mabadiliko ya Sheria ya Madini ya Mwaka 2010.
Baadhi ya Wabunge na Watendaji wa Wizara wakifuatilia semina kuhusu Sheri ya Madini ya Mwaka 2017.
Akizungumza katika semina hiyo, Katibu wa Tume ya Marekebisho ya Sheria Tanzania, Casmir Kyuki, alieleza kuwa, semina hiyo imelenga kuwaelemisha Wabunge kuhusu Sheria Mpya ya Madini ya mwaka 2017 baada ya kufanyika Marekebisho kadhaa katika Sheria ya Madini ya Mwaka 2010.
Aidha, pamoja na kupata elimu kuhusu sheria hiyo, wajumbe wa kamati hizo walipata fursa ya kuelimishwa kuhusu Kanuni Saba za Sheria ya Madini ambazo ni Kanuni ya Umiliki wa madini; Kanuni ya Biashara ya madini; Kanuni ya uendeshaji wa wananchi Kanuni ya madini ya mionzi.
Kanuni nyingine ni pamoja na Kanuni ya uongezaji thamani madini na Kanuni ya utafiti wa kijiolojia na Kanuni ya hifadhi ya ukaguzi wa hesabu na kumbukumbu.
Kwa upande wake, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Flurence Luoga aliwaeleza wabunge kuhusu sababu za maboresho ya Sheria ya Madini ya Mwaka 2010, Sheria ilimpa mwekezaji uhuru mkubwa ndani ya sekta ya madini.
"Uhuru huo ni pamoja na uhuru wa kuchimba , kusafirisha , kufanya uchenjuaji nje ya nchi, pamoja na kufanya tafiti bila kuwasilisha taarifa za kijiolojia na madini,"alieleza Luoga.
Akielezea juu ya sababu za kuwepo kwa uhuru huo katika sekta ya madini kabla ya maboresho ya Sheria ya 2018, Gavana Luoga alifafanua kuwa suala hilo lilitokana na Sheria zilizokuwepo tangu enzi za Serikali ya kikoloni.
Semina hiyo iliendeshwa na wabobezi wa masuala ya sheria , fedha na madini ambapo walitoa mada mbalimbali kuanzia historia ya mikataba ya kisheria ya kitaifa na kimataifa juu ya sekta ya madini tangu enzi za serikali za kikoloni za Ujerumani na Uingereza.
Watoa mada Wakuu katika semina hii walikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti Madini Tanzania (GST), Profesa Abdulakarim Mruma Profesa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Florence Luoga na Katibu wa Tume ya kurekebisha sheria Tanzania Casmir Kyuki.
Semina ilifanyika tarehe 19 Mei 2018, katika ofisi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndani ya ukumbi mdogo wa Pius Msekwa na kuhudhuria na kutoka Vyama mbalimbali vya siasa, Watendaji wa Wizara na Watalaam wa Sheria na Madini kutoka wizara ya Madini.
Na Samwel Mtuwa, Dodoma
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.