[Latest Updates]: Waziri Mavunde Akagua Ujenzi wa Jengo la Ghorofa Nane la Mafunzo ya Uongezaji Thamani Madini ya Vito

Tarehe : July 22, 2025, 10:41 a.m.
left

Bilioni 33 kukutumika kukamilisha Jengo la ghorofa pacha-TGC Arusha

Biashara ya madini kufanyika kwenye Jengo

Ni mkakati wa uongezaji thamani madini ya vito

Wachimbaji Arusha wamshukuru Rais Samia kwa miundombinu ya jengo

Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, leo Julai 22, 2025 ametembelea eneo la ujenzi wa jengo la kisasa la ghorofa nane la Kituo cha Jeomolojia Tanzania (TGC), linaloendelea kujengwa jijini Arusha, kwa lengo la kukagua maendeleo ya mradi huo muhimu kwa Sekta ya Madini nchini.

Katika ziara hiyo, Waziri Mavunde amepata fursa ya kujionea hatua mbalimbali za ujenzi na kupokea taarifa ya maendeleo kutoka kwa Mhandisi Julian Mosha wa Kampuni ya Skywards Lumocons Joint Venture pamoja na msimamizi wa mradi Jumanne Nshimba kutoka TGC ambapo baada ya kukamilika kwake unatarajiwa kuwa kitovu cha huduma za utambuzi wa madini, tafiti na mafunzo kuhusu vito vya thamani na madini mengine nchini, na hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia mnyororo wa thamani wa Sekta ya Madini.

Amesema Jengo hilo linatarajiwa kuwa na madarasa ya wanafunzi, karakana, mabweni ya wanafunzi, maabara ya madini pamoja na ofisi mbalimbali kwa ajili ya uongozi wa chuo hicho ambapo zaidi ya bilioni 33 zinategemewa kukamilisha mradi huo.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ukaguzi huo, Mhe. Mavunde ameeleza kuridhishwa na hatua iliyofikiwa lakini amemtaka mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi ili kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati na kwa viwango vilivyokusudiwa.

“Mradi huu ni wa kimkakati kwa mustakabali wa Sekta ya Madini nchini ambao utawaleta pamoja wafanyabiashara wa madini (One Stop Centre). Tunahitaji kuona ujenzi ukikamilika haraka ili Kituo hiki kianze kufanya kazi kama ilivyokusudiwa. Natoa wito kwa mkandarasi kuongeza nguvu kazi, vifaa na ufanisi ili kuendana na muda wa mkataba,” amesema Waziri Mavunde.

Mradi huo unatekelezwa chini ya usimamizi wa Wizara ya Madini kwa kushirikiana na taasisi ya TGC, ambapo jengo hilo litakapokamilika litaongeza uwezo wa kitaifa wa kuchambua madini, kutoa mafunzo ya kitaalamu, na kukuza ajira kwa vijana wa Kitanzania waliobobea katika masuala ya Jiolojia na Jiomolojia.

Aidha, Waziri Mavunde amesisitiza dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuimarisha miundombinu ya kisayansi na kiteknolojia kwa ajili ya matumizi bora ya rasilimali za madini na kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara na uongezaji thamani madini katika Ukanda wa Afrika.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Mwenyekiti wa Wachimbaji Mkoani Arusha (AREMA) Ndg. Alfred Mwaswenya na Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Madini (CHAMATA) Ndg. Jeremia Kituyo wamemshukuru Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa uamuzi wake wa ujenzi wa jengo ambalo litazalisha watanzania wenye ujuzi ya kuchakata madini ya vito lakini pia kurahisisha biashara ya madini kufanyika katika eneo hilo kwa kuwa litawakusanya wadau kwa wakati mmoja.

Akizungumza katika ziara hiyo,Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh.Kenani Kihongosi  ameipongeza Serikali kupitia wizara ya madini kwa ujenzi wa Jengo la kisasa la ghorofa nane la TGC ambalo litasaidia katika kuchochea biashara ya madini mkoani Arusha na kukuza uchumi wa wananchi wa Arusha.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals