[Latest Updates]: Mgodi wa Geita Watajwa Mfano Bora Kuhudumia Jamii

Tarehe : Oct. 2, 2022, 10:04 a.m.
left

Imeelezwa kuwa, Kampuni ya Uchimbaji dhahabu ya Geita Gold Mining Limited ( GGML) inaongoza kwa kuwa kampuni ya uchimbaji madini nchini inayofanya vizuri katika kutimiza Wajibu wa Makampuni kwa Jamii (CSR).

Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko alipotembelea mgodi wa GGM ili kushuhudia miradi mipya ya uchimbaji dhahabu inayofanyika katika mgodi huo Mkoani Geita.

"Mimi ningependa tuwe wa kweli, nchi hii kampuni inayofanya vizuri kwenye CSR kwenye madini ya kwanza ni GGM. Wamefanya kazi nzuri," amesisitiza Dkt. Biteko.

Ameongeza kuwa, kampuni hiyo imekuwa ikishirikiana na wananchi katika huduma mbalimbali kwa jamii zinazozunguka migodi hususan, katika ujenzi wa hospitali, shule, vifaa vya tiba ili jamii ipate huduma bora.

Aidha, ameipongeza GGM kwa kujenga mahusiano mazuri ya kijamii na wananchi wanaozunguka mgodi huo. Dkt. Biteko amepongeza GGM kwa kuweka mitambo mipya ya kuchenjua mabaki ya kaboni ili kupata dhahabu badala ya kusafirisha kaboni kwenda nje ya nchi kama ilivyokuwa hapo kabla.

Vile vile, mgodi wa GGM umeanza kuhama katika uchimbaji wa wazi na kwenda kwenye uchimbaji wa chini kwa chini (underground mining), ambapo tayari GGM imejenga mgodi wa chini ya ardhi na umeanza uzalishaji.

"Tunafurahi kuona kwamba mgodi wa GGM wamejitaidi kuendelea kuweka uzalishaji kuwa kwenye kiwango kinachotakiwa. Kwa mujibu wa taarifa za mgodi, mgodi huo unazalisha Wakia 480,000 hadi sasa, tunawapongeza sana," amesema.

Amesema, Serikali inaandaa Kanuni na Muongozo maalum ambao utawafanya watu wote watekeleze miradi ya kijamii bila kutegea nchini.

Naye, Makamu wa Rais wa Kampuni ya GGM, Simon Shayo akizungumzia kuhusu utekelezaji wa CSR kwa jamii  amesema, kampuni hiyo inaendelea kushirikiana na wananchi ili kujenga mahusiano mazuri katika mazingira yote yanayozunguka mgodi.

Pia, amemshukuru Dkt. Biteko  kwa kuipongeza GGM kwa namna kampuni hiyo inavyojitaidi kwenye kununua bidhaa na kutumia huduma za kitanzania.

"Asilimia kubwa ya bidhaa zetu sasa karibu asilimia 70 ya fedha inayotumiwa na GGM inanunua bidhaa kutoka Tanzania," amesisitiza.

Shayo amesema kuwa, lengo la kampuni ya GGM ni kuhakikisha kuwa inaendelea kuwa kinara kwa kufanya vizuri ili watu wavutiwe kuwa mwajiriwa wa GGM na wote wanaozunguka mgodi huo kuwa na ujirani wa manufaa.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Geita, Costantine Kanyasu ameeleza kuwa lengo ni kuona wananchi wanashiriki katika uchumi wa mgodi. Amesema katika maeneo mengi ya jimbo hilo mgodi unashirikiana na wananchi wake na kusisitiza kuwa jimbo linapokea  asilimia 54 ya fedha  ya CSR inayotengwa na kuzielekeza katika huduma za maendeleo.

 

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals