Tarehe : Sept. 3, 2025, 10:35 a.m.
Mwanza
Klabu ya Michezo ya Madini (MSC) inaendelea kuonesha makali yake katika mashindano ya 39 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yanayoendelea jijini Mwanza, baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1–0 dhidi ya Kilimo katika mchezo wa mpira wa miguu.
Mchezo huo uliopigwa leo, Septemba 3, 2025, kwenye uwanja wa sekondari ya Bwiru, uliiweka Madini katika nafasi nzuri ya kusogea hatua ya 16 bora, sambamba na timu ya kuvuta kamba wanawake ambayo nayo imeanza vyema.
Katika michezo ya awali, timu ya kuvuta kamba wanawake ya Madini iliibuka na ushindi wa mivuto 2–0 dhidi ya Uchukuzi, na kisha kuibamiza Tume ya Utumishi kwa ushindi wa mvuto 1–0. Matokeo hayo yameifanya Madini kuanza “kunusa” hatua ya mtoano kati ya timu 36 zinazoshiriki mashindano haya ya mwaka huu.
Mashindano yataendelea kesho ambapo Madini itavaana na Mahakama katika mpira wa miguu, huku timu ya kamba wanawake ikitarajiwa kutifuana na Wizara ya Ardhi.
Kwa mujibu wa upangaji wa makundi, timu ya Madini kamba wanawake ipo kundi B ikichuana na Uchukuzi, Haki, Ardhi na Tume ya Utumishi, wakati timu ya mpira wa miguu ipo kundi E ikipambana na OSHA, Mahakama, Kilimo na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.
Mbali na michezo hiyo, Madini pia imesajili ushiriki katika michezo ya ndani ikiwemo karata, drafti na bao, pamoja na riadha na mbio za baiskeli.
Mashindano ya SHIMIWI mwaka 2025 yanafanyika kwa kaulimbiu isemayo: “Michezo kwa Watumishi Huongeza Tija Kazini: Jitokezeni kushiriki Uchaguzi Mkuu 2025 kwa Amani na Utulivu
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.