[Latest Updates]: Dkt. Kiruswa Ashuhudia Utiaji Saini Mkataba Kati ya STAMICO na PLANTCOR

Tarehe : Feb. 25, 2026, 10:25 a.m.
left

DKT. Biteko awataka wananchi wa Bukombe kuchangamkia fursa

Dkt. Mwasse Mkataba kati ya STAMICO na PLANTCOR umelenga kuimarisha ushirikiano wa kimkakati

Shigella amesema Geita imebarikiwa aina mbalimbali za madini

Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Dkt. Steven Kiruswa, ameshuhudia Hafla ya Utiaji Saini wa mkataba wa ushirikiano kati ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na Kampuni ya Plantcor Mining and Plant Hire (Pty) Ltd kutoka Afrika Kusini kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa utafiti na uchimbaji wa madini ya dhahabu katika eneo la Kigosi, Wilayani Bukombe, Mkoa wa Geita.

Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt. Kiruswa amesema uwekezaji huo unatarajiwa kufungua milango ya ajira kwa wananchi wa Bukombe na mkoa wa Geita kwa ujumla, kuchochea ukuaji wa uchumi wa ndani na kuongeza mapato ya Taifa.

Amesisitiza umuhimu wa kampuni husika kutekeleza wajibu wake kwa jamii (CSR) pamoja na kuhakikisha ushirikishwaji wa wananchi katika mnyororo wa thamani wa sekta ya madini kupitia sera ya Local Content.

Ameeleza kuwa baada ya kukamilika kwa utafiti wa kijiolojia, Plantcor itawasilisha taarifa za kina za maeneo yanayozunguka mradi wa Kigosi ili kuwawezesha wachimbaji wengine wenye leseni katika eneo hilo kunufaika na taarifa hizo kwa maendeleo ya shughuli zao.

Aidha, Dkt. Kiruswa ameitaka Menejimenti ya STAMICO kushirikiana kwa karibu na Plantcor ili kuhakikisha mradi unasimamiwa kwa weledi, uwazi na kwa kuzingatia maslahi mapana ya Taifa. Vilevile, amewataka wawekezaji hao kutimiza ahadi zote za uwekezaji, uhamishaji wa teknolojia na kuzingatia Sheria za nchi ili mradi huo uwe mfano bora wa ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya STAMICO, Balozi Simon Sirro, amesema utiaji saini wa mkataba huo ni ishara ya kuimarika kwa mazingira ya uwekezaji nchini, akibainisha kuwa ubia huo unatekelezwa kwa mujibu wa Sheria huku maslahi ya wananchi yakilindwa kwa uwazi.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse, amesema mkataba huo unalenga kuimarisha ushirikiano wa kimkakati katika utafiti na uchimbaji wa dhahabu Kigosi. Ameongeza kuwa STAMICO inaendelea kuwa lango la kuvutia mitaji na teknolojia za kisasa kwa manufaa ya Taifa.

Amesema ushirikiano huo utawezesha kufanyika kwa tafiti za anga (airborne survey) zitakazohusisha matumizi ya ndege maalum kwa ajili ya uchunguzi wa kijiolojia, si tu katika eneo la STAMICO bali pia maeneo mengine ya Kigosi, hatua itakayowanufaisha wachimbaji wengi zaidi kupata taarifazakijiolojiakatika maeneo yao.

Mkurugenzi Mtendaji wa Plantcor, Joseph Wilmans, amesema kampuni hiyo ina uzoefu wa zaidi ya miongo miwili katika shughuli za madini kuanzia utafiti, uchimbaji, uchenjuaji hadi usambazaji wa bidhaa sokoni.

Amebainisha kuwa kampuni imeleta utaalamu wa kiteknolojia na kifedha utakaosaidia kuongeza uzalishaji na ajira kwa Watanzania, huku akiishukuru Serikali kwa kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Afrika Kusini.

Sambamba na hao, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigella, amesema mkoa huo umebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi za madini, na akamshukuru Rais kwa uamuzi wa kuufungua mradi wa Kigosi, hatua aliyosema imeendelea kuimarisha uchumi wa mkoa huo.

Naye, Mbunge wa Jimbo la  Bukombe na Naibu Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Dkt. Doto Biteko, ameipongeza STAMICO kwa kuimarisha ushirikiano huo na kuamua kusaini mkataba huo katika wilaya ya Bukombe.

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wachimbaji wa madini, hali inayowezesha wananchi kunufaika zaidi na rasilimali za Taifa.

Aidha, Dkt. Biteko amewataka wananchi wa Bukombe kuchangamkia fursa zitokanazo na uwekezaji huo na kutoa ushirikiano kwa wawekezaji ili kuhakikisha mradi wa Kigosi unakuwa chachu ya maendeleo endelevu kwa wilaya, mkoa na Taifa kwa ujumla.

Hatua ya utiaji saini mkataba huo imefanyika siku chache baada ya kampuni hiyo kukutana na Wizara ya Madini katika Kongamano la Indaba, ambapo ilitoa ahadi ya utekelezaji wa mradi huo mara baada ya mkataba kusainiwa, ikiwa ni ishara ya dhamira ya dhati katika kuimarisha ushirikiano huo.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals