[Latest Updates]: Spinel ya Mahenge Yawa Lulu Thailand.

Tarehe : Sept. 7, 2023, 2:19 p.m.
left

Bei yake kwa Sasa  Yatajwa ni Mara 10 Zaidi ya Tanzanite


Na Wizara ya Madini - Bangkok

Imeelezwa kuwa Madini ya Vito aina ya Spinel yanayochimbwa Mahenge Tanzania ni  miongoni mwa bidhaa inayotafutwa kwa kiasi kikubwa  na Wanunuzi na Wauzaji Wakubwa wa Madini ya Vito na Usonara wanaoshiriki na kutembelea katika Maonesho ya 68 ya Vito na Usonara yanayoendelea katika jiji la Bangkok eneo la Queen Sirikit nchini Thailand.

Hayo yamebainishwa Septemba 7, 2023 na Mkurugenzi wa Kampuni ya Ruby   International Limited Mhe. Salim Hasham ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ulanga, Mahenge Mkoa wa Morogoro ambaye kampuni yake inashiriki katika maonesho hayo. Kampuni hiyo inajishughulisha na uuzaji, uchimbaji na ununuzi wa madini mbalimbali ya vito yakiwemo ya Spinel, Tanzanite, Garnet na mengine.

Akizungumza katika mahojiano maalum, baada ya ujumbe wa Wizara kutembelea banda lake, Mhe. Salim amesema kwamba Spinel ni miongoni mwa madini yanayotafutwa zaidi katika soko la dunia yakiwemo madini ya Tanzanite ambayo yanayozalishwa Tanzania pekee ulimwenguni kote katika eneo la Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara.

Kufuatia mahitaji ya madini hayo kwenye soko la dunia, Mhe. Salim amewataka wachimbaji nchini kuinuka na kutumia maonesho makubwa ya madini yanayofanyika katika maeneo mbalimbali duniani kujitangaza, kutafuta masoko na kujenga mahusiano ya kibiashara na kusisitiza kuyaongeza thamani madini   yao  kwa lengo la kupandisha thamani yake  na hatimaye waweze kunufaika zaidi kupitia rasilimali madini, kuongeza  mapato ya Serikali na mchango wa Sekta ya Madini kwenye maendeleo ya nchi.

‘’Spinel inatafutwa sana hapa, kila anayekuja anauliza Mahenge Spinel? Ni madini yanayotakiwa sana kwenye soko la dunia. Isitoshe madini yanayozalishwa Tanzania ni maarufu sana duniani.   Ni kwetu sisi watanzania tuamue, tuamke na tufanye wenyewe  kwa kuwa tumeamua kufanya,’’ amesisitiza Mhe.Salim.

Ameongeza kwamba, Tanzania ni mzalishaji mkubwa wa madini ya Spinel, ikifuatiwa na nchi za Vietnam na Myanmar ( zamani Burma) na kuongeza kuwa, madini ya Tanzania katika soko la dunia yanachangia zaidi ya asilimia 15.

Akizungumza kuhusu thamani ya madini Spinel, Mthamini Mkuu wa Serikali kutoka Wizara ya Madini Archard Kalugendo amesema Spinel ni miongoni mwa madini yenye thamani kubwa duniani na kueleza kuwa, hivi sasa bei yake ni mara 10 zaidi ya Tanzanite.

Maonesho ya Bangkok ni moja ya maonesho makubwa na maarufu sana Barani Asia na sasa yana takribani miaka 40 tangu kuanzishwa kwake.  Serikali ya Tanzania inayatumia maonesho hayo kujitangaza, kutafuta masoko, ushirikiano, teknolojia mpya pamoja na kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu Sekta ya Madini hususan katika eneo la madini ya Vito na usonara ambapo nchi ya Thailand imepiga hatua kubwa katika uendelezaji wa madini hayo.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals