[Latest Updates]: Tanzania Yashika Nafasi ya Nne kwa Uwekezaji Sekta ya Madini Afrika

Tarehe : March 10, 2026, 9:06 a.m.
left

Ni ya 4 barani Afrika, nyuma ya Botswana, Morocco na Zambia

Alama ya Tanzania yapanda hadi 68.04 mwaka 2025 kutoka 62.75 (2024) na 46.38 (2023)

Tanzania yaorodheshwa nafasi ya 15 duniani kwenye Best Practices Mineral Potential Index kwa alama 75.00

Utafiti uliwahusisha wataalam na viongozi 2,304 wa kampuni za utafiti na uchimbaji.

Rais Samia apongezwa kwa mazingira mazuri ya Uwekezaji Tanzania


Tanzania imeendelea kuimarisha nafasi yake kama kivutio cha kimataifa cha uwekezaji kwenye sekta ya madini baada ya kuorodheshwa miongoni mwa maeneo yanayoongoza barani Afrika, kwa mujibu wa ripoti ya Fraser Institute, Annual Survey of Mining Companies 2025.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Tanzania imepata nafasi ya 34 kati ya maeneo 68 duniani yaliyotathminiwa katika Investment Attractiveness Index (IAI), kielezo kinachotumiwa na wawekezaji na kampuni za utafiti wa madini kuamua wapi waelekeze mitaji ya utafiti na maendeleo ya miradi.  

Katika muktadha wa Afrika, Tanzania imeendelea kushika nafasi ya juu kwa kuwa ya 4 barani Afrika katika IAI, ikifuata Botswana, Morocco na Zambia, hatua inayothibitisha ushindani wa Tanzania katika kuvutia mitaji ya kimataifa ya utafiti na uwekezaji wa madini.  

Ripoti inaonesha pia mwenendo chanya wa kupanda kwa alama za Tanzania, ambapo alama ya IAI imefikia 68.04 mwaka 2025, ikilinganishwa na 62.75 mwaka 2024 na 46.38 mwaka 2023 mwenendo unaoashiria kuongezeka kwa uaminifu na mvuto wa Tanzania kwa wawekezaji wa sekta ya madini.  

Kwa maelezo ya ripoti, IAI hujengwa kwa kuzingatia vipengele viwili vikuu vinavyoongoza maamuzi ya uwekezaji: uwezo wa kijiolojia wa rasilimali (mineral potential) na mazingira ya jumla ya kufanya biashara kwenye sekta husika. Ripoti hiyo inaeleza kuwa katika hesabu yake, asilimia 60 ya uzito huenda kwenye mineral potential na asilimia 40 huenda kwenye policy framework, ili kutoa taswira ya mvuto wa eneo husika kwa uwekezaji wa utafiti na uchimbaji.  

Katika kipengele cha Best Practices Mineral Potential Index kinachoangalia mvuto wa kijiolojia kama eneo lingekuwa na kanuni bora zaidi duniani Tanzania imeorodheshwa nafasi ya 15 duniani kwa alama 75.00, jambo linaloonesha kwa uwazi ukubwa wa fursa na uwezo wa rasilimali madini zilizopo nchini.  

Utafiti huu wa Fraser Institute ni miongoni mwa rejea muhimu zinazotumiwa kimataifa na sekta binafsi, taasisi za utafiti na wadau mbalimbali kutathmini mwenendo wa masoko ya uwekezaji wa madini. Kwa mujibu wa taarifa ya utafiti, dodoso lilipelekwa kwa viongozi na wataalam 2,304 wa kampuni za utafiti na uchimbaji, na waliotoa majibu waliripoti matumizi ya pamoja ya takribani Dola za Marekani bilioni 4.2 kwenye shughuli za utafiti wa madini mwaka 2025.  

Kwa Tanzania, nafasi hii inaongeza msukumo kwenye jitihada za Serikali za kuendelea kuimarisha sekta ya madini kama nguzo muhimu ya uchumi ikiwemo kuongeza utafiti, kuvutia mitaji mikubwa ya uendelezaji wa miradi, na kukuza ushiriki wa Watanzania katika mnyororo mzima wa thamani wa madini.  

Wataalamu wa uchumi na wadau wa sekta ya madini nchini wamempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuvutia uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya madini nchini Tanzania,huku wengi wakibashiri kuwa sekta ya madini kuwa nguzo kuu ya uchumi wa Tanzania kwa miaka michache ijayo.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals