[Latest Updates]: GST Kuanza Ujenzi wa Maabara ya Kisasa Geita

Tarehe : July 22, 2025, 10:34 a.m.
left

Tayari yakabidhi eneo la ujenzi.

Maabara hiyo itajumuisha Maabara tatu ndani yake.

Itakuwa mkombozi wa wachimbaji na wachenjuaji wa madini Kanda ya Ziwa na viunga vyake.

GEITA

Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) inatarajia kuanza ujenzi wa maabara ya kisasa katika eneo la Kanyala lililopo Halmashauri ya Mji wa Geita, mkoani Geita.

Maabara hiyo inatarajiwa kuwa ya kisasa itakayohudumia wadau wa uchimbaji na uchenjuaji madini katika mikoa iliyopo Kanda ya Ziwa.

Hayo, yamebainishwa leo Julai 22, 2025 na Mtendaji Mkuu wa GST Dkt.Mussa Budeba wakati akikadhi eneo maalum la ujenzi kwa mkandarasi.

Dkt.Budeba amemtaka mkandarasi huyo ambaye ni kampuni ya Brightwave kutumia muda uliopangwa katika mkataba kukamilisha kazi hiyo ya ujenzi. Aidha, Dkt. Budeba amemtaka mkandarasi huyo kuzingatia maadili na taaluma katika kutekeleza mradi huo ili Serikali na watanzania kwa ujumla watumie miundombinu hiyo kwa muda mrefu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho. 

Awali, akitoa taarifa kuhusu mradi wa  ujenzi wa maabara hiyo, Mkurugenzi wa Huduma za Maabara GST, Bw. Notka Banteze amesema kuwa, maabara hiyo ndani yake itakuwa na maabara tatu ikijumuisha Sehemu ya Shughuli za Uendeshaji na Utawala na eneo la Huduma ya Chakula.

Akielezea kuhusu huduma zitakazotolewa, Banteze amefafanua kuwa ni pamoja na  uchunguzi wa sampuli za miamba na madini,  tafiti za uchenjuaji madini, utambuzi wa madini na uchunguzi wa sampuli za mazingira kama vile sampuli za maji na mimea.

"Maabara hii itakuwa msaada mkubwa kwa wachimbaji na wachenjuaji madini, wachenjuaji madini wengi wanapoteza madini yao mengi kupitia marudio kwa kukosa uelewa wa namna bora ya kuchenjua madini kwa kuzingatia tabia za mbale". Aliongeza Banteze

Kwa mujibu wa historia ya maabara ya  GST ilianzishwa mkoani Dodoma mwaka 1926 na Serikali ya kikoloni ya Uingereza (British Oversees Manegement Authority  - (BOMA). Maabara hii imekuwa ikitoa huduma zake kutokea mkoani Dodoma tangu kuanzishwa kwake takribani miaka 100 iliyopita. Maabara hii itakayojengwa mkoani Geita itakuwa ya kwanza kutoa huduma za GST nje ya mkoa wa Dodoma.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals