[Latest Updates]: Nyongo ashuhudia Jiwe la Almasi la Uzito wa “Ct” 512.15 likiuzwa kwa Bilion 3, 262, 149, 332

Tarehe : May 25, 2019, 4:46 a.m.
left

Na: Issa Mtuwa (Wizara ya Madini) – Shinyanga

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, ameshuhudia mchimbaji mdogo wa madini ya almasi bwana Joseph akijizolea fedha, dola za kimarekani (USD) milioni 1, 418,510.82 ambazo sawa na Tsh. bilioni 3, 262,149,332.75 kutokana na mauzo ya jiwe moja lenye  uzito wa Kareti (ct)512.15. Shuguli ya mauzo ya Almas hiyo  imefanyika leo tarehe 25/05/2019 katika soko la Madini la mkoa wa Shinyanga na kushuhudiwa pia na Kamishna wa Tume ya Madini Prof. Mruma na vyombo mbalimbali vya usalama na wawakilishi wa benki ya CRDB Shinyangai. 

Akiongea wakati wa kushuhudia mauzo hayo , Naibu waziri Nyongo amesema, kutokana na mauzo hayo serikali  itapata USD 103,551.29 sawa na Tsh. milioni 238,136,901.61. Ameongeza na kusisitiza kuwa, adhima ya serikali ya awamu ya tano ni kuwezesha shuguli za wachimbaji wadogo na wadau wote  wa sekta ya madini kufanyika kwa utaratibu unao eleweka kwa faida yao na ya serikali.

“Nimpongeze bwana Joseph ambae anauza almasi yake hapa leo kwenye soko hili la madini, kila kitu kinakuwa wazi mbele ya serikali, polisi, watu wa usalama na wawakilishi wa Bank ya CRDB, bila usumbufu wowote, na hiki ndicho tunachokitaka sisi kama serikali, wachimbaji wote kufuata utaratibu tuliouweka.

Niwaombe wachimbaji kwa mara nyingine, acheni kuuza madini mchochoroni haita wasaidia zaidi ni kuhatarisha usalama wenu, na pengine hata kupunjwa kutokana na kuto kujua thamani halisi na bei ya madini yenu igeni mfano wa bwana Joseph, na niwaambie ukweli ukikamatwa unauza madini nje ya soko madini hayo yanataifishwa, hivyo utakuwa umekula hasara na utachukuliwa hatua za kisheria.” amesema Nyongo

Kwa upande wake Afisa msaminishaji madini kutoka tume ya Madini Bi. Dorcas Moshi, Mchambuzi na Mthamini wa Madini ya Vito na Almasi kutoka tume ya Madini aliekuwa anafanya shuguli nzima ya uthaminishaji wa Almasi hiyo, amefafanua kuwa fedha iliyopata serikali, Milioni 238,136,901.61 inajumuisha Mrabaha wa  USD 85,110.65 sawa na  Tsh. Milioni 195,728,959.97, Ada ya ukaguzi ni USD 14,185.11 sawa na Tshs. 32, 621, 493, .33 na Mrabaha wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu ilikotokea Almasi hiyo (Service Levy) ni USD 4,255.53 sawa na Tsh. 9, 786,448.

Kwa upande wake Kamishina wa Madini prof. Mruma amewasisitiza wachimbaji wadogo kuzingatia sheria na taratibu hususani kuchimba kihalali kwa kuhakikisha wanakuwa na leseni za uchimbaji na kulipa tozo zote za serikali kwani serikali ipo kwa ajili yao hivyo hawana sababu ya kuikwepa.

Kwa upande wake bwana Joseph mmiliki wa almasi hiyo, ameishukuru Wizara ya madini na Tume ya madini kwa utaratibu waliouweka katika kutoa muongozo na usimamizi wa namna ya mauzo ya madini unavyotakiwa kufanyika, ulinzi wa madini yao pindi wanapoyapata na ametoa wito kwa wachimbaji wadogo wenzake kuwa hakuna sababu ya kuyakimbia masoko yaliyoanzishwa na serikali kwani yanafaida nyingi ikiwemo usalama, ulinzi, uwazi na utambuzi wa thamani halisi ya madini kitu ambacho nadra sana kwenye masoko yasiyo rasmi.  

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals