Tarehe : Jan. 24, 2026, 4:57 p.m.
Mwenyekiti wa Bodi ya REA afurahishwa na STAMICO kuendelea kuboresha Ubora wa Rafiki Briquettes
Aelekeza Rafiki Briquettes kusambazwa zaidi kila kona ya Tanzania.
DG REA aahidi kuendeleza mashirikiano na STAMICO kwa kusaidia kwenye ujezi wa viwanda vingine vya Rafiki Brequettes
STAMICO kufanya uzinduzi wa viwanda viwili na kuanza ujenzi wa Kiwanda cha Geita- Ag MD
Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeridhishwa na hatua zinazofanywa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kuhakikisha upatikanaji wa Nishati Safi ya kupikia ya Rafiki Briquettes pamoja na kuendeleza kuboresha ubora wa Nishati hii. Sambamba na hayo imeridhishwa na kasi ya kuongeza idadi ya Viwanda vyake kufikia vinne ambapo viwili vya Kisarawe na Kiwira vikiwa vinafanya kazi kwa uwezo wa kuzalisha tani 20 kwa saa, kingine cha Tabora kikiwa katika hatua ya uzinduzi na Dodoma katika hatua ya usimikaji wa mitambo.
Akiongea baada ya ukaguzi wa Kiwanda cha Nishati Safi cha Rafiki Briquettes cha Kisarawe kinachomilikiwa na STAMICO, Mheshimiwa Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu, Mwenyekiti wa Bodi ya REA alisema“Mimi na wenzangu kwenye ziara hii tumefarijika sana kuona jinsi ambavyo wenzetu wa STAMICO walivyopiga hatua ya kujenga viwanda vya kuzalisha Nishati hii ya Rafiki Briquettes ambayo ni mbadala wa matumizi ya Nishati ambazo sio safi kama Kuni na Mkaa. Tumefarijika kuona mfumo mzima wa uandaaji wa Nishati hii na hatua amabazo STAMICO imekuwa ikizichukua kuendelea kuboresha Nishati hii. Kama walivyotuelezea, nishati hii inatokana na vumbi la Makaa ya Mawe (Coal dust) ambayo wanayapitisha kwenye mchakato wa kupunguza hewa za ukaa pamoja na kupunguza ukali wa uwakaji wake.
Tumeona kwamba pia wamefanya utaratibu wa kupata uthibitisho wa Ubora kutoka Shirika la Viwango la Taifa yaani TBS pamoja na kuweka mtambo mdogo wa utafiti ambao unaendelea kufanya tafiti mbali mbali kuhusiana na ubora pamoja na tachnolojia mpya. Tumeridhishwa pia na jinsi ambavyo wameweka utaratibu mzuri wa kuwafikia wateja ingawa nataka kuona wanaongeza kasi ili kuwafikia Watanzania wengi.
Tunajua ajenda kuu ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2034 Watanzania asilimia 80 wanakuwa wanatumia Nishati Safi"
Katika ziara hiyo Mhe Kingu aliambatana na Mha Hassan Saidy, Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mha Sophia Mgonja, Mjumbe wa Bodi, Bwn Stephen Mwakifamba, Mjumbe wa Bodi pamoja na viongozi na watumishi kadhaa kutoka REA. Lengo kuu la ziara hii ilikuwa kukagua kiwanda cha Rafiki Brequettes Kisarawe kuona shughuli nzima ya uzalishaji na ubora wa bidhaa unavyosimamiwa katika uzalishaji na pia kupata picha ya Kiwanda kipya ambacho REA wametoa ufadhili wa TZS Billioni tatu ambacho kitajengwa Geita.
Naye Mha Hassan Saidy, Mkurugenzi Mkuu wa REA ameitaka STAMICO kuangalia jinsi ya kuwafikia wananchi wengi kwa kuangalia wanavyoweza kushirikiana na Taasisi nyingine za binafsi ili kutekeleza kwa vitendo lengo kuu la kufikisha Nishati hii nchi nzima
Aidha alisema ili kufanikisha adhma ya kuifikisha Nishati Safi nchi nzima STAMICO haina budi kuangalia jinsi ya kushirikiana na taasisi nyingine binafsi ambazo zinaweza kusaidia kusambaza Nishati hii kwa kasi. Aliongeza kuwa REA ipo tayari kutoa ruzuku kwa Taasisi ambazo zinatengeneza majiko banifu ili wananchi wengi waweze kuyanunua na kuweza kutumia Nishati ya Rafiki Briquettes kwa ufanisi.
Alisema tayari REA wameshawapa STAMICO ufadhili kwa ajili ya kiwanda cha Geita na sasa wapo tayari kutoa ufadhili kwa Kiwanda kingine cha Tanga.
Awali akiwakaribisha na kuwasilisha taarifa ya mradi huu, Mha Baraka Manyama, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO aliwaelezea mipango ya Shirika ni kuhakikisha Nishati hii inasambaa nchi nzima.
Mha Manayma alisema STAMICO inaendesha viwanda viwili vikubwa vya Rafiki Brequettes vya Kisarawe na Kiwira na sasa Shirika lipo mbioni kuzindua Viwanda cha Tabora na Dodoma ambavyo vinatarajiwa kuanza Uzalishaji katika Mwezi Februari.
Aidha ameongeza kuwa ujenzi wa mitambo ya Kiwanda cha Geita umefika asilimia 50 wakati taratibu za kumpata mkandarasi wa ujenzi wa Kiwanda zikiendelea. Kwa upande wa Masoko, Mha Manyama aliwaeleza kwamba tayari taassi kama Magereza zote 129, Kambi za JWTZ,JKT, taasisi za elimu kwa maana ya shule na vyuo, hospitali, masoko ya kuchoma nyama, samaki pamoja na watu binafsi wanatumia Nishati hii ya Rafiki Briquettes.
Alisema Shirika limeshafanya majaribio ya kukausha mazao ya Chai na Tumbaku na yameenda vizuri.Tayari Wakulima wa Tumbaku wa Tabora wameeomba Nishati hii ipelekwe wanapoanza kuvuna zao hili mwishoni mwa mwezi wa Januari.
Sambamaba na hao pia kampuni kadhaa za Chai zimeshaanza kuagiza Nishati hii kwa ajili ya kukaushia.
Kwa upande wa masoko ya Kimataifa, Mha Manyama amesema tayari Shirika limeshafanya mawawasiliano ya kuwatembelea Jeshi la Magereza la Uganda na wamepanga kuja kutembelea Kiwanda Mwezi huu wa Februari.
Baada ya mazungumzo na mawasilisho hayo, Mwenyekiti wa Bodi, Wajumbe wa Bodi, Menejimenti na Watumishi wa REA walionyeshwa ufanishi wa Rafiki Briquettes kwa kuonyeshwa inavyochoma nyama, kuchemsha vyakula vigumu kama Makande, Kuchemsha Mahindi, kuonyeshwa vitu vya kukaanga kama Chips na Kuku pamoja na kuona mifumo ya majiko ambayo inaifanya Rafiki Briquettes iwe na ufanisi zaidi.
Viongozi hawa na Watumishi wa REA walifurahia chakula ambacho kiliandaliwa kwa kutumia Nishati hii ya Rafiki Briquettes.
Mhe Kingu aliwashuku STAMICO kwa makaribisho mazuri na kukiri kuwa Nishati hii ina nafasi nzuri ya kuwafikia watu wengi kutokana na gharama zake kuwa za kawaida. Alisisitiza STAMICO kuongeza kasi ya kuisambaza nchi nzima.
STAMICO Imejipanga kuendelea kuwa kinara wa kuhakikisha inashiriki kikamilifu katika kuzalisha Nishati hii safi ya Rafiki Briquettes ili kufikia lengo la kufikia asilimia 80 ya matumizi ya Nishati Safi ifikapo Mwaka 2034
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.