[Latest Updates]: Kampuni ya Uchimbaji wa Madini ya Makaa ya Mawe Ruvuma Zajivunia Kusaidia Jamii

Tarehe : May 22, 2025, 1:01 p.m.
left

Zatoa ajira 200 kwa vijana
Zachangia ujenzi wa zahanati

Ruvuma
 
Kampuni za uchimbaji wa madini ya makaa ya mawe katika Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma zimeendelea kusaidia jamii ambapo wananchi wanaoishi jirani na migodi wameendelea kunufaika na ajira huku migodi ikiendelea kuboresha huduma za jamii ikiwa ni pamoja na kuchangia ujenzi wa zahanati hali iliyopunguza adha ya wananchi kufuata huduma za afya katika maeneo ya mbali. 

Akizungumza katika mahojiano, Msimamizi wa Kituo cha Mauzo cha Kampuni ya Makaa ya Mawe ya Jitegemee (Jitegemee Holdings Company Limited), Mark Tarimo ameeleza kuwa katika miradi  iliyotekelezwa na kampuni hiyo kwa jamii ni pamoja na ujenzi wa vyoo vya shule katika kijiji cha Luagala pamoja na kutoa ajira kwa vijana zaidi ya 200 wanaozunguka maeneo ya mgodini kama mkakati wa kuwawezesha  kujikwamua kiuchumi na kupata unafuu wa maisha.

“ Vijana hawa tumeweza kuwapatia ajira  katika shughuli za udereva na kufunga maturubai kwenye magari yanayofika kupakia makaa,” amesema Tarimo.

Ameendelea kusema kuwa  kampuni ya Jitegemee imeweza kuboresha miundombinu ya mgodi ambapo kwa siku inaweza kuzalisha zaidi ya tani 3000 za makaa, ambayo huchakatwa na kuwauzia wananchi  huku wateja wao wakubwa ni kutoka nchi za Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.

Kwa upande wake Meneja wa kampuni ya Ruvuma Coal Limited, Sanzeh Ntikwa  akielezea namna mgodi ulivyoboresha huduma za jamii amesema  kuwa  mgodi umefanikiwa kujenga madarasa mawili kwenye kijiji cha Paradiso, zahanati na kuboresha ujenzi wa Soko la Paradiso pamoja na kununua vifaa vya michezo kwa vijana.

“Kwenye kijiji cha Sara tumeweza kujenga madarasa mawili, Ofisi ya walimu na zahanati kubwa, kwa sasa tumejipanga kujenga shule ya VETA kwenye kijiji cha Paradiso, ambapo tunasubiri vibali kutoka Serikalini pamoja na michoro ili tuanze ujenzi, vilevile tumenunua basi kwa ajili ya kuwabeba wanafunzi kutoka kijiji cha Paradiso kwenda kwenye shule iliyopo Luagala katika Wilaya ya Mbinga,” amesema Ntikwa.

Naye, Mjiolojia wa kampuni ya Ruvuma Coal Limited, Penina Rububula  ambaye ni mmoja wa wananchi walioajiriwa na mgodi huo akielezea manufaa ya ajira yake amesema  kupitia ajira yake ameweza  kusomesha watoto, kununua kiwanja pamoja na kuendesha maisha yake ya kila siku.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals