[Latest Updates]: Waziri Biteko awataka Mantra Tanzania kuipa muda Serikali kushughulikia ombi lao

Tarehe : Oct. 2, 2019, 6:49 a.m.
left

Waziri wa Madini Doto Biteko, ameitaka kampuni ya Mantra Tanzania kuipa nafasi ofisi yake ili kuweza kujiridhisha endapo maombi ya kusitisha kuanza kwa shughuli za uchimbaji wa madini hayo una tija kwa kampuni na Taifa.

Waziri Biteko ametoa kauli hiyo leo wakati wa kikao baina ya Wizara na uongozi wa Kampuni hiyo ulioitaka wizara kuridhia ombi la kusogeza mbele shughuli za uzalishaji wa madini hayo kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2020 mpaka 2024.

Akizungumza hoja hiyo iliyowasilishwa katika kikao hicho, Waziri Biteko alihoji uhakika bei ya madini hayo ifikapo mwaka 2024 katika soko la dunia la endapo utakuwa wakuridhisha na kuwataka kuwasilisha data zao ili ofisi yake iweze kuzifanyia kazi.

“Ni kiashira gani kinachowaonesha kuwa ifikapo 2024 kutakuwa na ongezeko la thamani kwa madini ya urani?” Biteko alihoji.

Aidha, Biteko aliutaka uongozi wa Kampuni hiyo kuwasilisha mchanganuo unaoonesha ongezeko la thamani ya madini ya urani ifikapo 2024 ili wataalamu wa wizara wafanyie kazi na kuishauri wizara juu ya kuridhia au kutoridhia maombi hayo.

Akizungumzia juu ya maamuzi yaliyofikiwa na kampuni hiyo, Rais wa Kampuni ya Mantra Tanzania, Vasiliy Konstantinov alisema bei ya kuuza madini hayo  kwenye soko la dunia imeshuka jambo ambalo litapelekea kampuni na serikali kutokunufaika na uwekezaji huo kutokana na kuwekeza kwa hasara.

Konstantinov alisema kuwa kampuni imeamua kufika na kukaa na wizara ili kupata msaada na kuhakikishiwa uhakika wa kuendelea na uwekezaji huo mara baada ya thamani ya madini hayo kuongezeka ili kuwawezesha kuwekeza kwa faida.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa leseni na Tehama kutoka Tume ya Madini, Yahya Samamba alihoji uamuzi wa Kampuni hiyo kuendelea na uwekezaji ifikapo 2024 endapo hakutokuwa na mabadiliko ya kuridhisha katika soko la dunia.

Akijibu hoja hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mantra Tanzania, Alexander Ryabchenko alisema kwa sasa kampuni hiyo iko katika utafiti wa kutafuta njia rahisi isiyotumia gharama kubwa za uwekezaji ili kuifanya kampuni hiyo kuendelea na uzalishaji mara baada ya muda huo kufika hata kama bei ya madini hiyo haitabadilika.

Mantra Tanzania ni kampuni ya uchimbaji mkubwa wa Madini nchini iliyotolewa na Wizara ya Madini mwaka 2013.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals