[Latest Updates]: Aliyoyasema Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa

Tarehe : Jan. 10, 2022, 2:41 p.m.
left

Kwa asili yangu ni mtendaji zaidi kuliko mzungumzaji. Namshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuniamini, na kunipanga kuja kufanya kazi pamoja nanyi naamini imani huzaa imani, nategemea nitarudisha imani kwa kufanya yale ambayo anategemea kuja kuyafanya hapa.

Nilishangaa kidogo kwa uteuzi kwasababu sikuwahi kujishughulisha na madini zaidi ya kuwatetea wachimbaji kwenye eneo langu.

Ni heshima kwangu katika kusaidia kusukuma gurudumu hili naamini nitajifunza mengi. Taaluma yangu ya awali ya Maendeleo ya Jamii ilifuata Model ya L3 kufanya maendeleo ya jinsi ya kuingia eneo jipya na unapofika unataza, unasikiliza na kujifunza hapa ndiyo ubunifu wako unaingia.

Nilipoingia hapa na mimi nimeona nyuso zinazokaribisha, kupokelewa vizuri, natarajia nitajifunza mengi na niko rahisi kufundishika.

Kila mahali nilipopita nilifanikiwa, kitu cha kwanza  kufanikiwa katika haya ni kufanya kazi kama timu, kupendana na cha tatu na muhimu sana ni kufanya kazi kwa bidi.

Nimekuja na mawazo yangu haya, tukiendana na haya naamini tutafanikiwa sana, lakini pia, mimi ni Mzalendo.

Inawezekana kuna madini mengi kwa kuwa tuna Taasisi ya Utafiti naamini tutafanikiwa kama Dubai na Mafuta. Kazi kubwa ambayo mimi natarajia ni kuwasaidia wachimbaji wajue rasilimali na wawe wabia katika shughuli hizo ili wazitumie kwa ajili ya kujenga nchi yetu na kutajirisha watanzania wote.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals