[Latest Updates]: Aliyozungumza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akifunga Mkutano wa Madini

Tarehe : Feb. 23, 2022, 12:29 p.m.
left

Niwapongeze kwa nia yenu ya dhati ya kushiriki katika Mkutano huu ulioambatana  na Maonesho ya Madini, hii inaonesha nia yenu ya dhati ya kushirikiana na Serikali katika kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha kuwa sekta hii ya madini inakuwa na manufaa makubwa kwa Wananchi na kwenye maeneo yote yanayotoa mchango wa madini ikiwa ni sehemu ya mchango wa uchumi wa Taifa letu.

Lakini pia niwapongeze na kuwashukuru Watendaji wote wa Kamati ya maandalizi kwa uratibu ba kufanikisha mkutano na maonesho haya ya kimataifa ya sekta ya madini mmefanya kazi kubwa na nzuri na sote tumeshuhudia mafanikio hayo

Nawashukuru Wageni wote kutoka nchi za nje, kuja kwenu kwenye mkutano huu mmeonesha manufaa katika tukio hili, niwahakikishie kwamba Tanzania ni nchi salama, na mtamaliza shughuli zenu salama na mtarudi nyumbani kwenu mkiwa salama.

Tanzania ni nchi iliyojaaliwa vivutio vingi vya utalii, baada ya kuhimisha mkutano huu nawaomba msirudi nyumbani kwanza tembeeleeni vivutio vyetu, tuna Mlima Kilimanjaro mlima mrefu kuliko yote Afrika, mlima ambao unaweza kuuona ukiwa kokote lakini ili kuupanda lazima uje Tanzania.

Tembeleeni pia Hifadhi za Wanyama zipo nyingi tu, Serengeti, Ngorongoro, Tarangire, Ruaha, Mikumi, Mwalimu Nyerere National Park na maeneo mengi tu mpaka Gombe kule Kigoma yana vivutio vingi tu, vuka Bahari pia Zanzibar kuna vivutio vingi sana.

Kipekee naomba nimpongeze Dkt Dotto Mashaka Biteko Waziri wetu wa Madini kwa kuhakikisha kwamba mkutano huu unaendelea luwa fursa kwa wadau wa sekta ya madini kila mwaka kukutana hapa na kubadilishana mawazo, uzoefu na kubainisha changamoto za sekta ya madini.

Nimeambiwa Mkutano wa mwaka huu umejadili kwa kina mazingira wezeshi kwa wawekezaji wetu, na kwamba mkutano huu umekuwa na manufaa makubwa sana kwa kukutanisha Serikali, Wachimbaji, Taasisi za fedha, wachenjuaji na wadau wote wa sekta ya madini, huu ni mwendelezo mzuri sana wa kuwaweka karibu na Serikali ili tufanye kazi pamoja.

Ndugu washiriki nimekuja na salamu zenu za kheri, za baraka na upendo kutoka kwa Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassam amenituma naomba pokeeni samalu zenu, lakini pia jamna mlikuwa hapa na Makamu wa Rais wakati akifungua mkutano huu, amenituma tena kuleta salamu zake kwenu.pokeeni salamu zenu kutoka kwa Dkt Philip Mpango.

Viongozi hawa wawili kwa pamoja wamenituma nije kuwahakikishia kuwa Serikali ya awamu ya sita iko bega kwa began a wadau wa sekta ya madini, Serikali hii inatambua mchango wenu na iko tayari kufanya kazi pamoja na nyie, itashirikiana na nyie katika Nyanja zote na hatimaye kuimarisha na kuendeleza sekta hii ya madini hapa nchini, kila mmoja kwa aina ya madini anayofanyia kazi.

 

Na mimi natumia nafasi hii pia kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan ambaye huwa anatoa maelekezo kwenye sekta ya madini kwa lengo la kuhakikisha kuwa wadau wa sekta hii ya madini wanapata kutumia nafasi hiyo kuboresha uchumi wao binafsi na Taifa kwa ujumla.

Serikali inayo nia ya dhati kuhakikisha inajua changamoto na kero mnazokutana nazo katika kazi zenu na kwamba Serikali ipo tayari kushirikiana na wadau wote ili kuzipatia ufumbuzi wake.

Zipo changamoto ambazo zinaweza kutekelezwa na watendaji wetu huko huko mliko lakini kuna changamoto za kuletwa huku kwenye ngazi ya Taifa ili tuzishughulikie, nataka niwahakikishie, yale yote yanayogusa ngazi ya juu tutayafanyia kazi.

Natamka haya ili kuwapa Imani kuwa serikali yenu ipo makini, ipo macho, na inafuatilia mwenendo wa sekta hii, wote mnatambua nilikuwa Mererani kuona maboresho tuliyofanya katika uchimbaji wa zao hili, na kupokea changamoto, na nimewaambia hapa kwenye mkutano huu imejitokeza changamoto ya masoko yake na mahali pa kufanyia kazi kufuatia kauli ile ya awali kwamba soko la Mererani liwe Mererani, nimewasikia na tutakutana Jijini Arusha tutazungumza hakuna kinachoshindikana.

Ndugu washiriki, nimefurahishwa sana na Kauli mbiu ya Mkutano wa Mwaka jhuu inayosema Mazingira Wezeshi ya Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini, Kauli mbiu hii ni thabiti na inasawiri azma ya Serikali ya awamu ya sita katika kuimarisha na kuendeleza sekta ya Madini hapa Nchini ambayo imekuwa ikitaka Wachimbaji wapate unafuu kupitia Sheria zetu na pale sheria inapokuwa ni kikwazo kuwepo fursa ili kuweka mazingira wezeshi.

Tumeshafanyamarekebisho mengi ya sheria kwenye sekta ya madini, sekta hii sasa inakua kwa kasi hata kwa mapato yanaenda vizuri, na tumefanya marekebisho hayo na kanuni zake kwa ushirikiano na nyie wadau, na mmeweza kutumia nafasi hii kubainisha changamoto za kisheria na sisi tunazichukua na tutazifanyia kazi.

Waziri wa Burundi amesema atakuja kujifunza Tanzania namna sekya ya madini inavyofanya kazi, na mimi nasema njoo tu maana hizi nchi mbili zina ushirikiano mkubwa, nasi tutakuja kujifunza kutoka kwenu.

Mkipata nafasi semeni tu, sekta ya madini ni kubwa  sana na tutaendelea kukutana  mara kwa mara kujifunza.

Tutaendelea kutenga maeneo na kuwapatia Leseni wachimbaji wadogo, FEMATA endeleeni kuratibu masuala ya wachimbaji wadogo.

Halmashauri tangazeni fursa za kiuwekezaji zilizopo kwenye maeneo yenu. Lengo ni kutumia rasilimali madini kwa manufaa yetu.

Wawekezaji leteni mitambo muwekeze kwenye uongezaji thamani madini muwekeze hapa nchini

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals