[Latest Updates]: GST yaagizwa kuandaa ramani za Madini ngazi za Mikoa, Wilaya

Tarehe : Nov. 12, 2018, 8:55 a.m.
left

  • Biteko asema wachimbaji sasa kuchimba kwa uhakika

Na Asteria Muhozya, Dodoma

Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania  (GST) imetakiwa kuandaa ramani zinazoonyesha madini mbalimbali katika ngazi ya Mikoa na Wilaya ili kuwapa nafuu watanzania wanaofanya shughuli za uchimbaji wa madini nchini.

Naibu Waziri Doto Biteko akimkabidhi Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia ya China, Profesa Sun Xiaoming Cheti cha kutambua mchango wake na kukamilika kwa utafiti wa Jiokemia uliofanywa nchini.[/caption]

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko   baada ya kupokea taarifa ya Utafiti wa Jiokemia katika skeli kubwa na skeli ndogo (Geochemical Mapping for High and Low Density) uliofanyika nchi nzima kwa ushirikiano kati ya GST na Taasisi ya Jiolojia ya China.

Naibu Waziri Doto, pia, ameitaka taasisi hiyo kuelekeza nguvu katika kuisaidia serikali katika kupata matokeo chanya katika shughuli za madini huku ikiongeza thamani ya kazi kutokana na utafiti huo na kuongeza kuwa, GST inaweza kutumia utafiti huo mkubwa kuandaa ramani za madini katika ngazi za Mikoa na Wilaya.

Akizungumzia manufaa ya tafiti huo kwa Tanzania, amesema baada ya muda si mrefu watanzania wanaofanya shughuli za uchimbaji watahamia katika uchimbaji wa uhakika na siyo wa kubahatisha kwa kuwa utafiti huo unaonesha mahali sahihi ambapo shughuli hizo zinaweza kufanywa.

Amesema mbali na shughuli za madini, utafiti huo pia unaweza kutumika katika sekta za kilimo, maji na ujenzi wa barabara kwa kuwa unawezesha kutambua aina ya udongo unaofaa kwa shughuli hizo.

Kutokana na umuhimu wa utafiti na kazi iliyofanywa na taasisi hizo mbili, Naibu Waziri Biteko ametoa wito kwa Watanzania kuitumia taasisi ya GST katika shughuli za kitaalam ikiwemo kupata taarifa za utafiti zinazohusu sekta ya madini na kuongeza kuwa, sekta hiyo inao uwezo mkubwa wa kutekeleza wajibu wake.

Aidha, Naibu Waziri Doto ametumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya China kutokana na ushirikiano huo iliyoutoa katika kutekeleza utafiti huo ambao umegarimu kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 4 na Laki Tano.

Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia ya China, Profesa Sun Xiaoming (kulia) akitoa taarifa ya utafiti huo. Katikati ni Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko na kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu, Mathias Abisai.[/caption]

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jilojia ya China, Profesa Sun Xiaoming amesema kuwa taarifa ya utafiti iliyowasilishwa ni ya nchi nzima ya Tanzania na eneo la Mkoa wa Mbeya.

Amesema utafiti huo umetoa matokeo ya jiokemia ya element 71 nchini kote na element 39 katika mkoa wa Mbeya na kuongeza kuwa utafiti huo utasaidia katika utekelezaji maendeleo ya shughuli za madini, kilimo na mazingira nchini.

Awali, akizungumza katika kikao hicho, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Mathias Abisai amesema kusudio la ujumbe huo ilikuwa ni kuhakiki kazi iliyofanyika na kuwasilisha ripoti. Ameongeza kuwa, ripoti hiyo itasaidia kwenye tafiti nyingine za madini ikiwemo maji na mazingira.

Ameongeza kuwa, mnamo Mwaka 2009 serikali ya China na Tanzania kwa kutumia taasisi zake za Jiolojia zilisaini hati ya makubaliano (MoU) kwa lengo la kuanzisha mradi huo wa miaka mitano ambapo kazi rasmi ya mradi ilianza mwaka 2013 na kukamilishwa mwaka 2018.

Naye, Kaimu Mtendaji Mkuu wa GST, Yokobeth Myumbilwa akileza malengo ya utafiti huo amesema kuwa ni kupata taarifa za utafiti wa jiokemia kwa ajili ya kuandaa kanzidata ambayo itaainisha uwepo wa taarifa zinazo ainisha uwepo wa aina mbalimbali za madini, upangaji miji ,pamoja na taarifa hizo kuweza kutumika katika shughuli mbalimbali katika  sekta za kilimo  na mazingira.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals