[Latest Updates]: Kitalu C Mirerani Chapata Mwekezaji Mzawa

Tarehe : Aug. 29, 2022, 10:44 a.m.
left

Asteria Muhozya na Tito Mselem - Mirerani

Serikali imesema tayari eneo la Kitalu C katika machimbo ya Tanzanite Mirerani limepata mwekezaji mpya Kampuni ya Franone Mining and Gems Co. Ltd inayomilikiwa na Watanzania wazawa kwa asilimia 100 baada ya kushinda Zabuni iliyotangazwa na Serikali mapema mwezi Mei, 2022.

Awali, eneo hilo lilikuwa likimilikiwa kwa ubia kati ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na wabia wenza chini ya Kampuni ya TanzaniteOne kwa asilimia 50 kwa 50  kabla ya Leseni ya umiliki wa eneo hilo kurejeshwa Serikalini.

Akizungumza katika Halfa ya Ununuzi wa Madini ya Tanzanite iliyofanyika katika Kituo chaTanzanite Magufuli Mirerani, Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko amemtaka mshindi  wa  zabuni hiyo kwenda kujitambulisha katika uongozi wa Mkoa wa Manyara, Wilaya wa Simanjiro na Tume ya Madini na kuongeza kuwa, maslahi ya wananchi wa Mirerani na taifa yatazingatiwa.

Akizungumzia biashara ya Tanzanite, Waziri Biteko amesema kuwa, mfumo unaotengenezwa na Serikali wa kujenga Tanzanite City ni  kuhakikisha biashara ya tanzanite inakuwa shirikishi na inafanyika kwa uwazi huku serikali ikilenga kumfanya mnufaika wa kwanza kuwa eneo hilo na taifa.

Akitolea mfano wa maeneo mengine ambayo yamenufaika na uwepo wa shughuli za madini  ameitaja Mikoa ya Geita, Shinyanga hususan Wilaya na Mkoa wa Kimadini wa Kahama kuwa imeendelea na kupata manufaa makubwa ya kiuchumi na kijamii kutokana na  namna migodi  inavyowajibika kwa jamii  kutokana na huduma zinazotolewa  katika maeneo yanayozunguka migodi na kuongeza kuwa,  matarajio ya Serikali ni kuona eneo la Mirerani linanufaika ipasavyo na madini hayo kama ilivyo kwa mikoa hiyo.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Christopher Ole Sendeka ameipongeza Serikali kwa kutangaza zabuni ya wazi ya kitalu C ambayo pia ilihusisha vyombo vya ulinzi na usalama katika ufuatiliaji wake na kuongeza kwamba, wana Simanjiro wana imani na wamiliki wapya wa eneo hilo.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere akizungumza katika hafla hiyo amesema changamoto zote zilizowasilishwa na mbunge huyo katika kuendeleza biashara ya tanzanite zitafanyiwa kazi na kuongeza kwamba tayari ujenzi wa Kituo cha Tanzanite City umefikia hatua kubwa.

Kwa upande wake,  Rais wa Chama cha Wachimbaji  Madini Tanzania (FEMATA) John Bina amesema   tukio la kumpata mchimbaji mwingine mwingine aliyechimba madini ya tanzanite yenye uzito mkubwa  ni kiashiria kwa Serikali kuona umuhimu wa kuwaendeleza na kuwawezesha wachimbaji wadogo kwa kuwa manufaa wanayoyapata yanatumika hapa  hapa nchini kukuza na kuendeleza shughuli nyingine.

Ameiomba Serikali kuendelea kuzihamasisha taasisi za fedha kutoa mikopo kwa wachimbaji wadogo na kueleza kwamba, wachimbaji wadogo wanahitaji teknolojia za kisasa ili waweze kuchimba kwa tija na mafanikio.

 

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals