Tarehe : April 19, 2025, 7:17 p.m.
Timu ya Wanawake ya Madini Sports Club imeendelea kung'ara katika michuano ya kuvuta kamba inayoendelea mkoani Singida, baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya timu ya wanawake ya Maji Sports Club katika mchezo wa kusisimua na wa aina yake.
Katika awamu ya kwanza ya mchezo huo, Madini walionesha nguvu na umahiri mkubwa kwa kuwavuta wapinzani wao ndani ya dakika mbili tu. Hata hivyo, awamu ya pili ilikuwa ngumu, ambapo timu ya Maji walifanikiwa kuwavuta Madini kwa shida, hali iliyosababisha kila timu kujinyakulia pointi moja hivyo kugawana alama kwa sare ya 1-1.
Mchezo huo ulikuwa ni wa mwisho kwa upande wa hatua ya makundi kwa timu ya wanawake, na kwa matokeo hayo, Madini Sports Club wametinga hatua ya robo fainali, wakiwa miongoni mwa timu 8 bora.
Kwa upande wa wanaume, Madini Sports Club walitarajiwa kucheza dhidi ya timu ya Wizara ya Viwanda, lakini mchezo huo haukufanyika baada ya wapinzani wao kushindwa kufika uwanjani, na hivyo Madini kupewa ushindi wa pointi 2 mezani.
Timu ya wanaume bado inaendelea na michezo ya makundi hadi tarehe 20 Aprili 2025 ambapo itajulikana kama watajiunga na wenzao katika hatua ya mtoano.
Mashindano hayo hufanyika kila mwaka kwa lengo la kuimarisha mshikamano miongoni mwa wafanyakazi, kukuza afya kupitia michezo, na kuenzi uzalendo na mafanikio ya kazi kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.