[Latest News]: Madini Yaanza Maandalizi Mpango Mkakati wa Miaka 10

Tarehe : May 9, 2023, 11:51 a.m.
left

Leo Mei 9, 2023 Katibu Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali amekutana na kuzungumza na Washauri wa kodi kampuni ya PricewaterhouceCoopers Limited (PWC), Deloitte Tanzania na KPMG katika kikao kifupi kuhusu maandalizi ya Mpango Mkakati wa Miaka 10 wa Wizara ya Madini jijini Dar es Salaam.

Aidha, kikao hiki kimefuatia maelekezo ya Mhe. Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko aliyoyatoa hivi karibuni wakati akimtambulisha Katibu Mkuu kwa watumishi wa wizara ya Madini.

Kikao hicho kimezungumzia pia kuhusu shughuli mbalimbali za uchimbaji wa madini zinazofanyika na matarajio ya Sekta ya Madini katika kipindi cha miaka 10 ijayo 

Wengine waliohudhuria kikao hicho ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Dkt. Mussa Budeba, Mkurugenzi wa Sera na Mipango Augustine Ollal, Kamishna wa Msaidizi wa Madini Maruvuko Msechu, Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara ya Madini Tume ya Madini Venance Kasiki na Kaimu Meneja Uwekezaji na Mipango STAMICO Nsalu Nzowa.

 

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals