Tarehe : June 13, 2023, 6:03 p.m.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Juni 13, 2023 amehutubia kwa njia ya Mtandao Mkutano wa Kimataifa wa Taasisi ya Uwazi na Uwajibikaji katika Sekta ya Madini, Mafuta na Gesi Asilia (EITI) unaondelea Jijini Dakar nchini Senegal chini ya udhamini wa Rais Mackey Sall, Bodi ya EITI na wadau wa Sekta za Uziduaji.
Katika hotuba yake fupi aliyowasilisha mbele ya washiriki zaidi ya 1,500 toka zaidi ya nchi 90 duniani; Rais Samia amesisitiza umuhimu wa wavunaji wa Rasilimali za madini kuhakikisha kuwa Uwekezaji wao unawanufaisha wananchi wanaoishi katika maeneo husika na taifa kupitia uwekaji wazi wa uzalishaji wao na mchango stahiki katika mapato ya taifa. Kwa sasa nchi 57 duniani ni wanachama hai wa EITI.
Ujumbe wa Tanzania uliowakilisha taifa kwenye Mkutano huo unaongozwa na Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa na wajumbe sita ambao ni Kamishna wa Madini Dkt. Abdulrahaman Mwanga, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Danstan Kitandula, Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Jesica Kishoa.
Wengine ni Bi Mariam Mgaya, Kaimu Mtendaji wa TEITI, Ndugu Ludovic Utouh, Mwenyekiti wa Kamati ya TEITI na Ndugu Adam Anthony, Mjumbe wa Kamati ya TEITI.
Mkutano huu ambao ulifunguliwa na Waziri Mkuu wa Senegal pia ulihudhuriwa na Mawaziri Wakuu toka nchi mbalimbali sambamba na waliohudhuria kwa njia ya mtandao akiweko Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza, Tony Blair.
Mkutano huo utaendelea kesho tarehe 14/6/2023 ambapo ujumbe wa Tanzania utawasilisha mada kuhusu fursa za uwekezaji katika Sekta ya Madini Mkakati.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.