[Latest Updates]: Waziri Mavunde Aeleze Mchango wa Marehemu Edson Nkongo Sekta ya Madini

Tarehe : March 15, 2025, 1:03 a.m.
left

Awaongoza Waombolezaji kumuaga nyumbani kwao Kibamba

Abainisha namna alivyosaidia kuongeza mapato ya Sekta kutokana na mifumo aliyoianzisha na wenzake, umo wa LUKU

Kaimu Katibu Mkuu Asema – Alikuwa mwenye bidii ya kazi, mwadilifu

Mchungaji Asema Amefanyika Baraka kwa Watanzania ndani ya muda mfupi

Dar Es Salaam

Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, ameuelezea mchango mkubwa wa aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Wizara ya Madini Marehemu Edson Nkongo katika kuboresha na kuongeza Makusanyo ya Maduhuli ya Sekta ya Madini.

"Edson kwa kushirikiana na wenzake, alianzisha mifumo bora ukiwemo wa Masoko ya Madini, ambao umeleta mageuzi makubwa katika ukusanyaji wa maduhuli na kueleza kuwa umesaidia kuongezeka kwa makusanyo ya maduhuli kutoka shilingi bilioni 116 hadi kufikia shilingi bilioni 753 katika Mwaka wa Fedha 2023/24 ,  na kuongeza mwaka huu tunatarajia kukusanya shilingi trilioni moja," amesema Waziri Mavunde.

Ameyasema hayo leo Machi 15, 2025 wakati akitoa Salam za rambirambi  za Wizara  kumuaga mtumishi huyo aliyefariki dunia Machi 12, 2025 katika  Hospital ya Tumbi- Kibaha  alipokuwa akipatiwa matibabu na kusema, Edson anabaki kuwa nguzo  kuu kwenye mabadiliko  ya Sekta ya  Madini na kwamba utaalam wake  umeisaidia nchi.

‘’Edson alikuwa mbunifu aliyejua anachopaswa kufanya, atabaki kwenye kumbukumbu zetu. Kupitia yeye na wenzake, amesaidia kuongeza mapato ya sekta kutokana na mifumo aliyoianzisha, hali ambayo ilifanya nchi nyingi kuja nchini kujifunza,’’ amesema Waziri Mavunde.

Ameongeza kwamba mbali ya mifumo inayotumiwa katika Sekta ya Madini, pia alihusika katika kamati za kitaifa kuandaa mifumo mingine ikiwemo mfumo wa Luku wa Tanesco na kuongeza, Serikali na Wizara tumepata pigo,’’ amesema Waziri Mavunde.

Akisoma wasifu wa marehemu Edson kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Madini Augustine Olal amesema  marehem Edson  alifanya shughuli za mfano ikiwemo kuanzisha mfumo wa Local Content kwa kushirikiana na wenzake na kumweleza kuwa alikuwa mtumishi mwenye bidii ya kazi na mwadilifu.

Olal ametoa shukrani kwa familia ya marehemu, Hospital za Mlonganzila, Regency, Mloganzila na Tumbi Kibaha alikopatiwa matibabu.

Naye, Mchungaji Petro Lazaro aliyeongoza ibada ya mazishi akizungumza katika ibada hiyo amewataka waombolezaji kuishi maisha ya unyenyekevu na kuwatumikia wengine.

‘’Edson ameacha somo la maisha tunayopaswa kuishi kama watu tunaomtumaini Mungu, amefanyika baraka kwa watanzania kwa muda mfupi, hii ni kutokana na namna waombolezaji walivyomwelezea ikiwemo wasifu uliosomwa,’’ amesema mchungaji Lazaro.

#Apumzike kwa Amani, Amina.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals