[Latest Updates]: Madini ya Almasi Yenye Thamani ya Ths Bilioni 1.7 Yakamatwa Yakitoroshwa Mwanza

Tarehe : May 23, 2025, 1:04 p.m.
left

Waziri Mavunde awapongeza RC Mtanda,Kamati ya Usalama,Uwanja wa Ndege na Kikosi kazi Madini

Aelekeza uchunguzi zaidi kubaini mtandao wote wa wahusika

Atoa rai kwa wadau wa madini kuzingatia sheria ya biashara ya madini nchini

Raia wa Kigeni mwenye asili ya India ashikiliwa 

Mwanza

Madini ya almasi yenye thamani ya zaidi ya Sh1.7 bilioni yamekamatwa yakitoroshwa kupitia Uwanja wa ndege wa Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari ljumaa usiku,Mei 23, 2025, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema madini hayo yalikamatwa Mei 18, 2025 kwa ushirikiano kati ya vyombo vya ulinzi na taasisi mbalimbali za Serikali na kutumia fursa hiyo kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. Said Mtanda,Vyombo vya usalama,uongozi wa uwanja wa Ndege wa Mwanza na Kikosi Kazi cha Wizara ya Madini kwa kazi kubwa na ya kizalendo ambayo wameifanya.

“Mtu mmoja raia wa kigeni ambaye ana asili ya India , anashikiliwa kwa mahojiano kuhusiana na tukio hilo na anatarajiwa kufikishwa mahakamani uchunguzi na taratibu

Katika tukio hilo,almasi ghafi yenye uzito wa karati 2,729.82 na thamani ya takriban USD 635,887.66 (sawa na Shilingi za Kitanzania 1,715,434,129.67) yaligunduliwa yakiwa yamefichwa kwenye mabegi manne na raia mmoja mwenye asili ya India kwa lengo la kuyasafirisha bila vibali halali wala kufuata taratibu za kisheria.

Nitoe rai kwa wadau wote wa Sekta ya Madini nchini kuhakikisha wanafuata sheria ya biashara ya madini nchini Tanzania ili wasipate hasara kwa kupoteza madini hayo ambayo hutaifishwa na serikali” Alisema Mavunde

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Saidi Mtanda amesema Mkoa wa Mwanza unaendelea kuimarisha ulinzi na udhibiti wa biashara zote haramu ili kuhakikisha nchi yetu ya Tanzania inanufaika na rasilimali madini.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals