Tarehe : March 21, 2024, 1:19 p.m.
●Kuongeza wataalam wa uongezaji thamani madini
● Kuongeza idadi ya viwanda vya uongezaji thamani madini nchini
● Kuanzisha maabara za Madini ya Vito katika Mikoa yenye Madini
Na.Samwel Mtuwa - Arusha
KATIKA Kutekeleza Sheria ya Madini ya mwaka 2010 na marekebisho yake ya 2017 inayozuia madini ghafi kusafirishwa nje ya nchi, Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) kimejipanga kuhakikisha Sekta ya Madini inaendelea kuimarika kwa uongezaji thamani madini ndani ya nchi ili kuendelea kuleta faida zaidi.
Hayo yamebainishwa leo Machi 21, 2024 na Kaimu Mratibu wa Kituo hicho Mha. Ally Maganga wakati akizungumza na waandishi wa habari waliopo katika ziara ya kutembelea miradi ya Kituo hicho kilichopo jijini Arusha.
Maganga amesema kuwa ili kufanikisha hilo, kituo cha TGC kinaendelea kupanua wigo wa utoaji mafunzo ya uongezaji thamani madini ili kuwepo na vituo na viwanda vingi vya uongezaji thamani nchini.
Maganga ameeleza kuwa kitaalam madini yaliyoongezewa thamani yana bei mara dufu ukilinganisha na madini ghafi hivyo lengo la Sheria hiyo ni kuhamasisha ujenzi na uanzishaji wa viwanda vya uongezaji thamani madini nchini jambo ambalo TGC imejipanga kutekeleza ili kuongeza fursa za ajira kwa vijana pamoja na kuleta fedha za kigeni nchini kupitia mauzo ya madini yaliyoongezewa thamani nje ya nchi.
“Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 na marekebisho yake ya Mwaka 2017 hairuhusu kusafirisha Madini ghafi nje ya nchi, hii ni kwasababu yanakwenda kutengeneza ajira nje, lakini kwa upande mwingine Sheria hii inachochea ajira nchini kwani kuna vijana wanapata ajira hapa kwenye Kituo chetu, kwenye taasisi nyingine za Serikali na nje ya Kituo na wengine wanapata fursa kwenye viwanda ambavyo vinachakata madini hayo,” amesema Maganga.
Maganga amefafanua mkakati mwingine ni kuwapeleka vijana katika nchi ambazo Wizara ina mashirikiano ya kikazi ikiwemo Thailand ili kuwapa utaalam na uzoefu zaidi katika mnyororo mzima wa uongezaji thamani Madini.
Maganga aliendelea kusema kuwa Eneo mahsusi ambalo Kituo pia kimejipanga kulitekeleza kikamilifu ni kufungua maabara za Madini ya Vito na metali za thamani kwenye maeneo yenye SHUGHULI za Madini ikiwemo Dar es salaam Ili kurahisisha, kuongeza tija na kuwahakikishia wananchi thamani halisi ya bidhaa wanazonunua.
Mikakati mingine ni pamoja na ujenzi wa jengo la kisasa litakalo kuwa na ghorofa nane (8), kutanua wigo wa kutoa huduma za maabara, kuanzisha makumbusho ya madini ya vito na kitengo cha utafiti wa Madini ya Vito.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.