[Latest Updates]: TEITI Yatoa Elimu kwa Wadau na Washiriki Katika Jukwaa la Uziduaji 2025

Tarehe : June 19, 2025, 1:46 p.m.
left

 TEITI kuweka wazi ripoti yake ya 15 kabla ya tarehe 30 Juni, 2025

 Uwazi wa Mikataba na ujenzi wa regista ya Majina ya wamiliki wa Kampuni katika Sekta ya uziduaji waanza kutekelezwa 

 Dodoma 

Imeelezwa kwamba, tangu Tanzania ijiunge na Asasi ya Kimataifa ya EITI iliyopo nchini Norway, imetoa kwa umma ripoti 14 za TEITI kwa kipindi cha kuanzia Julai 2008 hadi Juni, 2022. Aidha, kwa sasa TEITI ipo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha ripoti ya 15 ya TEITI kwa kipindi cha mwaka 2022/2023 ambayo itawekwa wazi kwa umma kabla ya tarehe 30 Juni, 2025. 

Hayo, yameelezwa leo Juni 19, 2025 na Kaimu Meneja wa Kitengo cha Uwazi na Uwajibikaji kutoka Taasisi ya TEITI - Bw. Erick Ketagory alipo mwakilisha Katibu Mtendaji wa Taasisi ya TEITI katika Jukwaa la Uziduaji la mwaka 2025 linalofanyika Jijini Dodoma. Jukwaa hilo limeandaliwa na Asasi ya Kiraia ya Hakirasilimali.

Bw. Ketagory amesema kuwa, TEITI imeanza kutekeleza takwa la uwekaji wazi wa Mikataba ambayo Serikali imeingia na Kampuni za Madini, Mafuta na Gesi Asilia ambapo Mikataba hiyo inapatikana katika tovuti ya TEITI.

Akielezea kuhusu uwekaji wazi wa majina ya wamiliki wa makampuni katika Sekta ya Madini, Mafuta na Gesi Asilia, TEITI imekamilisha ujenzi wa Rejista husika(Beneficial Ownership Register) ambayo ipo wazi kwa matumizi ya umma ambayo inapatikana kupitia bo.teiti.go.tz.

Bw. Ketagory amesisitiza kuwa Milango wa TEITI ipo wazi kwa ajili ya  kushirikiana na wadau mbalimbali ili kutekeleza kikamilifu matakwa ya Sheria inayosimamia TEITI na vigezo vya Kimataifa vya EITI.

 Zifuatazo ni picha katika Matukio.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals