[Latest Updates]: STAMIGOLD, GST Zatakiwa Kufanya Tafiti za Kina Biharamulo

Tarehe : May 19, 2023, 3:02 p.m.
left

Mbibo Asisitiza Afya, Usalama Mahala pa kazi

STAMIGOLD Yaajiri Watanzania 566

Takriban kilo 50 mpaka 60 Zinazalishwa na Stamigold kila mwezi

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo ameitaka Kampuni ya STAMIGOLD kushirikiana na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kufanya tafiti za kina ili kubaini maeneo mengine yenye mashapo kwa lengo la kuongeza maisha ya Mgodi wa Biharamulo Mine ambapo kwa sasa maisha ya mgodi huo ni miaka mitano.

Imeelezwa kuwa, uzalishaji wa dhahabu katika mgodi huo unazidi kuimarika mwaka hadi mwaka ambapo kwa sasa zaidi ya kilo 50 mpaka 60 zinazalishwa kwa mwezi ikilinganishwa na kilo 35 mpaka 40 za dhahabu kwa miaka iliyopita.

Mbibo ameyabainisha hayo  kwenye ziara yake ya kikazi katika mgodi wa Biharamulo Mine baada ya kupata nafasi ya kuzungumza na watumishi katika mgodi huo.

Mgodi wa Stamigold-Biharamulo unamilikiwa kwa asilimia mia na Stamigold ambayo ni Kampuni tanzu ya Shirika ya Madini la Taifa (STAMICO) inayojishughulisha na uchimbaji wa madini ya dhahabu katika wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera.

Pamoja na hayo, Mbibo amesema afya na usalama mahali pa kazi ni jambo muhimu ambalo linapaswa kuzingatiwa na watu wote hususan katika maeneo yenye shughuli za uchimbaji madini.

Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa Stamigold-Biharamulo Mine Ally Ally amesema mgodi huo unachimbwa na Watanzania kwa asilimia mia ambapo imeajiri watumishi 566 ikiwa 232 wameajiriwa na Stamigold, 238 na wanafunzi kutoka vyuo vikuu na taasisi za elimu.

Pamoja na mambo mengine, Ally amesema Mgodi wa STAMIGOLD unampango mkakati wa kuongeza uzalishaji kwa kununua mashine za uchimbaji na upakiaji kwa lengo la kuongeza tija na ufanisi katika shughuli zao ikiwa ni pamoja na kuchimba kwa faida ambapo kwa sasa vifaa hivyo hukodishwa kutoka kwa wakandarasi.

 

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals