[Latest Updates]: GST na BGS ya Uingereza Zasaini Hati ya Makubaliano ya Utafiti wa Madini

Tarehe : May 22, 2025, 12:59 p.m.
left

London

 Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na Taasisi ya Jiolojia ya Uingereza (BGS) zimesaini makubaliano ya ushirikiano katika maeneo mbalimbali ikiwemo ya tafiti za madini.

Hati ya Makubaliano (MoU) hayo imesainiwa leo Mei 22, 2025 jijini London Uingereza na kushuhudiwa na Ujumbe kutoka Tanzania ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo pamoja na Balozi wa Tanzania nchini humo Mhe. Mbelwa Kairuki.


 Akizungumza baada ya kusaini makubaliano hayo ambayo pia yamefanyika Kwa njia ya mtandao, Mtendaji Mkuu wa GST Dkt. Mussa Daniel Budeba amebainisha maeneo ya ushirikiano  kuwa ni pamoja na kufanya tafiti za madini;   vifaa vya teknolojia ya kisasa na uchunguzi wa sampuli za madini maabara.

Dkt. Budeba ametaja maeneo mengine ya ushirikiano  ni kufanya miradi ya pamoja katika utafiti wa jiolojia, jiokemia, utafiti wa jiofizikia kwa kutumia ndege, ugani wa jiolojia, ufuatiliaji na usimamizi wa masuala ya majanga asili ya jiolojia, usimamizi wa taarifa za jiosayansi na masuala ya kimazingira na mafunzo kwa watumishi na kubadilishana uzoefu.

Aidha, Dkt. Budeba ameongeza kuwa, makubaliano hayo yatakuwa na manufaa kwa pande zote mbili ambapo Tanzania itanufaika na ujuzi na teknolojia mpya katika kufanya tafiti za madini, huduma za maabara na usimamizi wa taarifa za jiosayansi.

Awali, akifungua hafla hiyo ya utiaji Saini Makubaliano hayo, Naibu Katibu Mkuu Mbibo amezishukuru pande zote mbili kwa kufanikisha kuandaa Hati hiyo na kuahidi kutoa ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha shughuli hiyo muhimu.

#InvestInTanazaniaMiningSector
 Vision2030:MadininiMaishanaUtajiri

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals