[Latest Updates]: Madini yamuaga Mtumishi wake

Tarehe : June 26, 2023, 12:31 p.m.
left

Kamishna wa Madini Dkt. Abdulrahman Mwanga amempongeza Mtumishi wa Wizara hiyo Joseph Manaku kwa kulitumikia Taifa kwa weledi na uzalendo mkubwa hadi kufikia muda wake wa kustaafu Utumishi wa Umma.

Dkt. Mwanga ametoa pongezi hizo katika hafla fupi ya kumuaga mtumishi huyo iliyoandaliwa na Idara ya Madini katika viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma.

Dkt. Mwanga amesema, Manaku ni mtu wa upendo, mshikamano na mpenda haki, ambapo Wizara hiyo bado inamuhitaji lakini kutokana na Sheria inabidi astaafu utumishi wa umma.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Wizara ya Madini Nsajigwa Kabigi amewataka watumishi wa Wizara hiyo kuiga mazuri yote aliyoyafanya Manaku ili kuleta maendeleo na tija katika utumishi wao.

Naye, Joseph Manaku amewashukuru watumishi wa Wizara ya Madini na Taasisi zake kwa mkupa ushirikiano wa kutosha katika kipindi chote cha utumishi wake katika wizara hiyo na kuwaomba kuendelea kushirikiana kwenye shida na raha katika kipindi chake chote cha utumishi wao.

Hafla hiyo ya kumuaga Manaku imewashirikisha viongozi mbalimbali wa Wizara ya Madini na Taasisi zake.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals