[Latest Updates]: Bilioni 51.42 Zakopeshwa kwa Wachimbaji Wadogo 127

Tarehe : July 4, 2025, 12:18 p.m.
left

GEITA

Imeelezwa kwamba katika kipindi cha mwezi Julai 2024 hadi Machi 2025 jumla ya shilingi bilioni 51.42 zilikopeshwa kwa wachimbaji wadogo wa madini 127 kutoka katika Taasisi mbalimbali za fedha nchini ikiwa ni juhudi za kuwapatia mtaji  wachimbaji wadogo walio jisajii katika vikundi mbalimbali nchini.

Hayo yamesemwa leo Julai 6, 2025 na Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Dkt. Steven Kiruswa wakati anafunga rasmi mafunzo ya ukuzaji ujuzi kwa wachimbaji wadogo wa madini 467 yaliyoandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kwa kushirikiana na Wizara ya Madini. 

Dkt. Kiruswa amesema kuwa,  Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kutekeleza mkakati wa kuwawezesha wachimbaji wadogo kwa kuwapatia ujuzi ili kuongeza tija, usalama na ufanisi katika shughuli zao za uchimbaji madini.

Amefafanua kuwa, Serikali inatambua na kuthamini mchango wa wachimbaji wadogo wa asilimia  40 ya maduhuli yatokanayo na uzalishaji wa madini nchini, hivyo itaendelea kuwajengea uwezo wa kila namna pamoja na kuendelea kuwapatia vifaa vya utendaji kazi kama itakavyohitaji.

Awali, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bi. Alana Nchimbi, amesema tangu kuanza kwa utekelezaji wa Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi mwaka 2016, mpaka  sasa, Serikali imetumia  kiasi cha shilingi Bilioni 111.3 ambacho kimewawezesha wanufaika 157,909.

Aidha, ameongeza kuwa, kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 Serikali ilitenga jumla ya shilingi Bilioni 10.8 kwa ajili ya utekelezaji wa Programu hiyo ambapo jumla ya wanufaika 10,786 wamefaidika na 479 ni wachimbaji wadogo wa Mkoa wa Geita.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Wachimbaji Wadogo wa Madini Mkoa wa Geita, Bw. Titus Kabuo, ameishukuru serikali kwa kuendelea kuwa karibu na wachimbaji wadogo kupitia mafunzo ya ukuzaji ujuzi. 

Amesema juhudi za Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Wizara ya Madini zimeonyesha dhamira ya kweli ya kuwawezesha wachimbaji kufanya kazi kwa weledi.

Mafunzo hayo ya wiki moja yaliwashirikisha wachimbaji wadogo zaidi ya 200 kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Geita. Washiriki walipatiwa mafunzo ya nadharia na vitendo kuhusu mbinu bora za utafutaji na uchimbaji wa madini, matumizi sahihi ya vifaa na kemikali, utunzaji wa mazingira, pamoja na afya na usalama kazini.

#MineralValueAddition
#InvestInMiningSectprTz
GDP:10.1 From MineralSector

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals