[Latest Updates]: RC Dodoma Ailika STAMICO Kuwekea Kwenye Madini ya Mkoani Kwake

Tarehe : Aug. 7, 2025, 11:14 a.m.
left

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, ametoa wito kwa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kuwekeza kikamilifu katika rasilimali za madini zinazopatikana katika Mkoa huo na kusisitiza kuwa hatua hiyo itasaidia kuongeza thamani ya madini, kutoa ajira kwa wananchi na kuchochea maendeleo ya uchumi wa Mkoa na taifa kwa ujumla.

Senyamule ametoa wito huo alipotembelea katika banda la STAMICO wakati wa Maonesho ya Kilimo ya NaneNane yanayoendelea jijini Dodoma.

Akizungumza baada ya kukagua shughuli na bidhaa zinazotolewa na STAMICO, Senyamule ameeleza kuwa Mkoa wa Dodoma umebarikiwa kuwa na aina mbalimbali za madini, ikiwemo madini ya Gypsum, Chokaa, Manganese, Shaba pamoja na madini ya ujenzi kama kokoto na mchanga na kusema kuwa uwekezaji wa STAMICO unaweza kusaidia kufungua fursa mpya za kiuchumi kwa wakazi wa Mkoa huo na kutoa mchango mkubwa katika pato la taifa.

"STAMICO ni taasisi ya serikali yenye uwezo mkubwa wa kitaalamu na kifedha, hivyo naiomba itumie fursa hii kuwekeza zaidi hapa Dodoma. Tuna rasilimali nyingi ambazo bado hazijachunguzwa wala kuendelezwa ipasavyo. Ushirikiano wa karibu kati ya serikali ya Mkoa na STAMICO unaweza kuleta mapinduzi katika sekta ya madini,” amesema Senyamule.

Kwa upande wake, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa STAMICO Bibiana Ndumbaro amemweleza Mkuu wa Mkoa kuwa Shirika hilo tayari limeanza Uchimbaji na uuzaji wa kokoto jijini Dodoma.

 Ameongeza kuwa Shirika linaendelea kufanya utafiti kwenye maeneo yake mbalimbali ya uwekezaji katika madini ya kimkakati nchini, huku Dodoma ikiwa miongoni mwa maeneo yenye vipaumbele kutokana na utajiri wa rasilimali madini zilizopo.

Maonesho ya Nanenane ni jukwaa muhimu la kuonesha teknolojia na fursa mbalimbali katika sekta za kilimo, ufugaji, viwanda na madini, na huwakutanisha wadau kutoka sekta za umma na binafsi. Shirika la STAMICO ni miongoni mwa taasisi zinazoshiriki kikamilifu katika maonesho hayo kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi kuhusu shughuli zake na fursa zilizopo katika sekta ya madini.

Mkoa wa Dodoma unaendelea kuimarika kama kitovu cha maendeleo nchini, na uwekezaji katika sekta ya madini unatarajiwa kuwa miongoni mwa nguzo muhimu za kukuza uchumi wa mkoa huo katika miaka ijayo.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals