[Latest Updates]: Wawekezaji watakiwa kujitokeza uwekezaji wa jasi Itigi

Tarehe : April 20, 2020, 10:26 a.m.
left

Na Greyson Mwase, Singida

Wawekezaji wa Madini wametakiwa kujitokeza katika uwekezaji kwenye shughuli za uchimbaji wa madini ya jasi katika eneo la Itigi Wilayani Manyoni Mkoani  Singida kwa kuwa madini hayo ya ubora wa kipekee hususan katika utengenezaji wa saruji.

Wito huo ulitolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Itigi, Ally Minja alipokuwa akizungumza  kwenye ziara ya Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Tume ya Madini  na waandishi wa madini katika mkoa huo yenye lengo la kuangazia mafanikio ya Sekta ya Madini katika mkoa wa Singida.

Alisema katika eneo la Itigi kuna jasi  yenye ubora na ya kutosha isipokuwa kumekuwepo na maeneo mengi ambayo hayajaombewa leseni za madini hayo.

Aliongeza kuwa, mkoa wa Singida una miundombinu ya kutosha kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za uchimbaji wa madini ya jasi na kusafirisha mikoani na katika nchi za jirani ya Tanzania.

Katika hatua nyingine, Minja aliwataka wananchi wanaoishi katika vijiji vyenye maeneo ya mchanga kuomba leseni kwa ajili ya kuchimba madini hayo, kuchimba na kujipatia kipato huku wakilipa kodi mbalimbali Serikalini.

Akielezea hali ya uwekezaji katika halmashauri ya Itigi, Minja alisema kuwa kwa sasa kumeanzishwa viwanda kwa ajili ya kutengeneza chaki na urembo na kuongeza kuwa malighafi nyingine zimekuwa zikipelekwa katika mkoa wa Simiyu kwa ajili ya kutumika kwenye viwanda.

Wakati huohuo Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Rahabu Mwagisa akielezea manufaa ya  Sekta ya Madini  wilayani humo alisema kuwa ni pamoja na uwepo wa ajira kwenye shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu na jasi,  uwepo wa viwanda vya kutengeneza chaki na Serikali kupata kodi mbalimbali.

Katika hatua nyingine aliongeza kuwa, Serikali ya wilaya inatarajia kuanzisha vituo vya ununuzi wa madini ya dhahabu ili kusogeza huduma karibu na wachimbaji wa madini kabla ya madini hayo kuuzwa kwa wafanyabiashara wakubwa wa madini.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals