[Latest Updates]: Rais Samia Azindua Mitambo ya Uchorongaji Madini

Tarehe : Oct. 21, 2023, 4:21 p.m.
left

Zaidi ya Shilingi bilioni 9.2 zatumika kununua mitambo STAMICO

Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa  Tanzania  Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan  leo Oktoba 21, 2023 amezindua  Mitambo Mitano (5) ya Uchorongaji kwa ajili ya Wachimbaji Wadogo pamoja na vifaa kazi vingine vya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) vyenye jumla ya thamani ya shilingi 9,178,559,128.

Uzinduzi huo umefanyika katika Kituo cha Mkutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma  ambapo umeenda sambamba na kukabidhi vifaa hivyo kwa wachimbaji  Wadogo wakiwemo Shirikisho la Wachimbaji Wadogo Tanzania (FEMATA) na Chama cha Wachimbaji Wanawake Tanzania (TAWOMA) ambapo  vinajumuisha Mitambo  Mitano ya uchorongaji  yenye thamani ya Shilingi bilioni 2.22.  

Vile vile, Vifaa vingine ni pamoja na Lori tatu za kubeba vifusi vya madini (Dump trucks) zenye thamani ya Shilingi milioni 544, Lori moja la kubeba mitambo (Lowbed) lenye thamani ya Shilingi milioni 274, Mtambo mmoja wa kusaga makaa ya mawe (Coal crusher) wenye thamani ya Shilingi bilioni 1.58.

Vifaa vingine ni Mtambo mmoja wa kusaga miamba kwa ajili ya kokoto (stone/aggregate crusher) wenye thamani ya Shilingi bilioni 1.137, Mtambo mmoja wa kufua upepo yaani Air compressor wenye thamani ya Shilingi milioni 424, Lori moja la kubebea maji (water bowser) lenye thamani ya Shilingi milioni 210.

Aidha, Mitambo miwili ya uzalishaji wa Mkaa Mbadala (Rafiki Briquettes) wenye uwezo wa kuzalisha tani 20 kwa saa yenye thamani ya Shilingi bilioni 2.396, Magari mawili (2 hardtop) kwa ajili ya shughuli za uzalishaji madini migodini yenye thamani ya Shilingi milioni 317 na Jaw Crusher 10, Metal Detector (20) na Injini ya Dizeli aina ya 24HP Moja (1) vyote vikiwa na thamani ya Shilingi milioni 72.5.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals