[Latest Updates]: GST, TFRA, na TFS Zasaini Hati ya Makubaliano Mkakati wa Kuzalisha Mbolea

Tarehe : Jan. 25, 2024, 9:13 p.m.
left

Mbolea kuzalishwa nchini kwa kutumia Malighafi za ndani

Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imesaini hati ya makubaliano (MoU) na TFRA pamoja na TFS ya Mkakati wa kuzalisha mbolea kwa kutumia malighafi zinazopatikana nchini.

Hafla ya utiaji saini imefanyika leo januari 25, 2024 katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Kilimo uliopo Jijini Dodoma.

Akizungumza kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa GST, Kaimu Meneja wa Huduma za Jiolojia Bw. Maswi Solomon amesema, GST  imeingia kwenye makubaliano hayo kwa lengo la kutafiti na kubainisha maeneo yapatikanayo madini mbolea ili kuja na mkakati wa uzalishaji wa mbolea kwa kutumia malighafi zipatikanazo nchini.

Aidha, Bw. Maswi amesema, GST haiishii kwenye utafiti pekee ila pia kuainisha sehemu zinazopatika madini mbolea na kushauri nini kifanyike baada ya kugundua maeneo yapatikanayo malighafi hiyo.

Kwa Upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni la mbolea (TFS) Samwel Mshote amesema, lengo la kusaini makubaliano hayo ni kuangalia ni kwa namna gani taasisi hizo zitashirikiana ili kupata malighafi kwa ajili ya kuzalisha mbolea kwa soko la ndani na nje ya nchi.

Sambamba na hayo, Mshote amesema, mahitaji ya mbolea ni makubwa ambapo zinahitajika tani milioni moja ambapo 10% inazalishwa ndani ya nchi na 90% inazalishwa nje ya nchi.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mamlaka ya Udhibiti wa mbolea Nchini (TFRA) Bw. Joel Laurent amesema, Tanzania ukiweza kuzalisha Mbolea ndani ya nchi, mahitaji ya fedha za kigeni yatakuwa yatapungua kwa kiasi kikubwa kuliko ilivyo sasa.

Awali, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Mweli alizipongeza taasisi zilizoshiriki katika hafla hiyo na kuwataka kuhakikisha wanetekekeza kwa vitendo maazimio yote ya kikao hicho.

Pamoja na mambo mengine, hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Madini, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Nishati, GST,  TPDC, NDC, STAMICO, Tume ya Madini na TANESCO.

#vision2030MadininiMaishanaUtajiri#

#UtafitiwaMadiniTanzania

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals