[Latest Updates]: GST Yafanya Mageuzi Makubwa Sekta ya Madini

Tarehe : March 27, 2025, 10:55 a.m.
left

Mafanikio ya Miaka Minne ya Serikali ya Awamu ya Sita 2021-2025 

GST YAFANYA MAGEUZI MAKUBWA SEKTA YA MADINI

Na.Samwel Mtuwa - Dodoma

Katika kipindi cha miaka minne cha Serikali ya Awamu ya Sita, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imefanikiwa kufanya mageuzi mbalimbali katika nyanja ya utafiti , upimaji wa sampuli za madini na  utoaji mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa madini nchini.

Hayo yameelezwa leo tarehe 27 Machi 2025 na Kaimu Mtendaji Mkuu wa GST , Notka Banteze wakati akiongea na waandishi wa habari katika Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dodoma.

Banteze amesema kuwa, mafanikio hayo yametokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali  kwa lengo la  kuona GST inaimarika zaidi kwa ukuaji endelevu wa sekta ya madini.

Akizungumzia kuhusu maendeleo ya tafiti za jiolojia , jiokemia na jiofizikia amesema mpaka kufikia mwaka 2024 , utafiti wa madini ya viwandani ulikamilika  ambapo jumla ya madini viwanda 44 yalibainishwa.

Sambamba na hapo, GST imefanikiwa kufanya utafiti wa madini ya helium  katika mikoa ya Arusha , Manyara, Dodoma, Singida na Shinyanga na kubaini kiwango cha helium katika chemchem za majimoto zinazofaa kwa hatua ya utafiti wa kina katika maeneo ya Ziwa Natron na Eyasi.

Kwa upande wa machapisho ya utafiti , Banteze amesema GST imefanikiwa kuchapisha vitabu viwili ambavyo ni kitabu cha madini yapatikanayo Tanzania toleo la tano  pamoja na kitabu cha madini viwanda toleo la pili pamoja ramani za maeneo husika.

Akielezea kuhusu mafunzo kwa wachimbaji wadogo, Banteze amesema GST imekamilisha utoaji wa mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa madini 2733
yaliyohusu uchukuaji wa sampuli wakilishi na utambuzi wa jiolojia ya maeneo yenye uwepo wa madini katika mikoa ya Lindi,Morogoro,Geita na Mwanza.

Banteze amefafanua kuwa, mwelekeo wa Serikali kupitia GST katika mwaka 2025/2926 kuwa,  GST imepanga kufanya utafiti wa kina kw kutumia ndege ili kuongeza asilimia  za utafiti wa kina kutoka asilimia 16 mpaka 34 , ikiwa na lengo la kufikia asilimia 50 ifikapo mwaka 2030.

GST imepanga 
kujenga maabara ya kisasa (state of art labaoratory) katika mkoa wa Dodoma kwa ajili kuimarisha uchunguzi wa  sampuli za madini nchini ili kuchochea shughuli za utafiti nchini na hivyo kuhamasisha ukuaji wa Sekta ya Madini. Maabara husika itakuwa na vifaa vya kisasa na itaweza kufanya uchunguzi wa sampuli za madini nyingi zaidi ikiwemo zinazojumuisha madini muhimu na kimkakati.

Aidha, GST imepanga kujenga majengo ya kisasa ya maabara na ofisi katika mikoa ya Geita na Mbeya ili kuwasogezea huduma karibu zaidi wachimbaji madini ikiwemo wachimbaji wadogo wa madini. Kukamilika kwa ujenzi huo kutaongeza tija kwa wachimbaji wa madini kwa kuwapunguzia kuchimba kwa kubahatisha. 

Pamoja na mambo mengine, Banteze amesisitiza kuwa GST imekusudia kukamilisha ujenzi wa mfumo wa usimamizi wa taarifa na takwimu za Taifa za madini. Kukamilika kwa mfumo huo utaongeza ufanisi katika utunzaji na usambazaji wa taarifa za madini na hivyo kuchochea uwekezaji katika sekta ya madini

Awali, akifungua mkutano huo mkurugenzi Idara ya Habari (Maelezo) Rodney Thadeus ameipongeza GST kwa kazi nzuri inayofanya kwa maendeleo ya taifa na jamii kwa ujumla katika kuelekea Dira ya Taifa ya mwaka 2050.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals