[Latest Updates]: Soko la Madini Laanzishwa Tanga Kusogeza Huduma kwa Wachimbaji

Tarehe : Sept. 18, 2025, 12:10 p.m.
left

 Mnyororo wa Thamani wa Madini Kubaki Tanga Kupitia Soko la Madini

 Fursa Mpya kwa Wachimbaji Wadogo kuuza Dhahabu na Vito kwa bei stahiki na usalama wa uhakika.

Tanga, 

Imeelezwa kuwa kuanzishwa kwa Soko la Madini linalojumuisha madini ya dhahabu na vito lililoanzishwa mjini Tanga, linatarajiwa kuwa jukwaa la moja kwa moja kwa wachimbaji wadogo wa madini kuuza bidhaa zao kwa usalama na kwa bei stahiki sambamba na kuwaondolea usumbufu wa kusafiri umbali mrefu kufuata masoko ya madini hayo.

Hayo yalibanishwa na Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Tanga, Mhandisi Laurent Bujashi, wakati akizungumza na Madini Diary jijini humo mapema wiki hii, na kueleza kuwa lengo kuu la kuanzishwa soko hilo ni kuwasogezea karibu huduma wachimbaji wa madini na wafanyabiashara wa madini na kuhakikisha kuwa madini yote yanayozalishwa mkoani humo yanafanya mnyororo wa thamani kubaki Tanga. 

“Soko hili pia litakuwa kituo cha taarifa kwa wachimbaji na watumiaji wa madini, likiwezesha kutangaza bidhaa za dhahabu na vito zinazozalishwa hapa mkoani Tanga,” alisema Bujashi.

Aidha, Mhandisi Bujashi alibainisha kuwa soko hilo litasaidia kuondoa mianya ya utoroshaji wa madini ambayo mara nyingi hupelekea hasara kwa Serikali na wachimbaji wadogo na kwamba kuanzishwa kwa soko hilo kunatarajiwa pia kuongeza mapato yatokanayo na Sekta ya Madini mkoani Tanga, huku likiwa ni chachu ya ukuaji wa biashara na uwekezaji katika sekta hiyo.

“Wachimbaji wa madini tunawakaribisha kuleta dhahabu na vito ili kuyauza kwa utaratibu ulio rasmi, huku wakipata faida zaidi na usalama wa kibiashara. Soko hili linatarajiwa kuwa kiini cha maendeleo ya madini mkoani Tanga na kuimarisha mnyororo wa thamani ndani ya Mkoa” aliongeza Bujashi

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Wafanyabiashara wa Madini mkoani humo, Mndambi Mrinji, alisema kuwa kuanzishwa kwa soko hilo ni matokeo ya kilio chao cha muda mrefu. 

“Hizi ni juhudi za Afisa Madini Mkazi kuanzisha soko hili kwa lengo la kuhakikisha huduma zinakuwa katika eneo moja hapa (centralized) jirani na Ofisi ya Afisa Madini Mkazi na zinapatikana kwa urahisi. Tunaishukuru Serikali kwa hatua hii inayosaidia wachimbaji wadogo kama sisi,” aliongeza Mndambi.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals