[Latest Updates]: POSCO Yadhamiria Kuongeza Uwekezaji Tanzania

Tarehe : March 9, 2024, 1:27 p.m.
left

Seoul, Korea Kusini

Katika hatua ya kuongeza Uwekezaji na kuimarisha ushirikiano wa biashara kimataifa  Kampuni ya  kimataifa inajishughulisha na uzalishaji wa bidhaa zitokanazo na madini ya chuma ijulikanayo kama POSCO yenye makao makuu yake nchini Korea Kusini, imedhamiria kuongeza uwekezaji katika sekta ya madini nchini Tanzania.

Hayo yamebainishwa katika mkutano wa Madini Muhimu na Mkakati kwa Bara la Asia na Afrika wakati wa uwasilishaji mada juu ya jiolojia ya Tanzania kwa Taasisi ya Jiosayansi na Madini ya nchini Korea Kusini (KIGAM)  uliofanyika jijini Seoul nchini Korea Kusini. 

Katika Mkutano huo Kampuni ya Kimataifa ya POSCO iliueleza ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo kuwa wamedhamiria kuongeza uwekezaji nchini Tanzania hususani kwenye bidhaa zinazotengenezwa kwa kutumia Madini Muhimu na ya Mkakati.

Kampuni ya POSCO ilieleza kuwa kwasasa wameingia ubia na kampuni ya uchimbaji madini ya Black Rock ambayo ina ubia na Serikali ya Tanzania kwenye mradi wa uchimbaji wa madini ya Kinywe wilayani Mahenge yaani Mahenge Graphite Mine. 

Kwa upande wake , Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo aliihakikishia kampuni ya POSCO kuwa Serikali ya Tanzania itatoa ushirikiano wa kutosha na wa kila namna itakapohitajika kwasababu sekta ya madini Tanzania inahitaji wawekezaji makini na wenye uzoefu kama kampuni ya POSCO.

Sambamba na mkutano huo ujumbe wa Tanzania ulipata fursa ya kutembelea maonesho ya kimataifa ya Korea yajulikanayo kama  EV TREND KOREA  kwa lengo la kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni ya POSCO.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals