Tarehe : June 16, 2025, 12:56 p.m.
Ni kupitia Mafunzo yanayotolewa na Kituo cha TGC
Mwanza
Wadau mbalimbali wanaoshiriki katika Jukwaa la Nne la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini wameonesha kufurahishwa na fursa zilizopo kwenye mnyororo wa thamani madini ya vito walipotembelea banda la Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) ambapo wameelezwa pia kuhusu fursa za mafunzo zinazotolewa na kituo hicho.
Jukwaa hilo linafanyika jijini Mwanza katika Viwanja vya Malaika Beach Resort, limeanza leo Juni 16, 2025 na linatarajia kuhitimishwa Juni 18, 2025 ambalo linahusisha wadau wakiwemo kutoka kampuni za uchimbaji, watoa huduma migodini, taasisi za Umma, na wengine.
Katika jukwaa hilo linakwenda sambamba na maonesho ya madini, TGC ni miongoni mwa taasisi chini ya wizara zinazoshiriki ambapo kimepata wasaa wa kuelimisha kuhusu mafunzo na huduma mbalimbali zinazotolewa na kituoni hapo.
Mafunzo yanayotolewa na kituo hicho ni kuanzia ngazi ya cheti na diploma katika huduma za utambuzi madini ya vito, utengenezaji wa tuzo (trophy) za miamba na vito, ukataji madini ya vito, pamoja na utengenezaji bidhaa za usonara.
Wadau wanakaribishwa kutembelea banda laTGC, kujiunga na mafunzo hayo kwa kujaza fomu za maombi zinazopatikana katika banda la TGC na kwenye tovuti www.tgc.ac.tz. au kupitia namba +255 737 816 121.
#Uongezajithamani kwa Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii
#ValueAddition for SocioEconomic Development
#Wekeza katika Uongezaji thamani Madini
#InvestInTanzaniaMiningSector
#MadininiMaishanaUtajiri
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.