[Latest Updates]: Baraza la Dhahabu Duniani (WGC) Laonesha Utayari wa Kushirikiana na Tanzania Kukuza Uwekezaji Nchini

Tarehe : Feb. 13, 2026, 11:04 a.m.
left

Wachimbaji wadogo kujengewa uwezo wa kuzalisha zaidi dhahabu

Wafurahishwa na Programu ya MBT ya wanawake na Vijana

WGC kusaidiana na serikali kurusha satelaiti ya utafiti wa madini wa kina

Prof. Kitila awaalika wawekezaji kuongeza thamani madini nchini

Serikali ya Tanzania na Baraza la Dhahabu Duniani(WGC) na Kampuni ya Usafishaji dhahabu ya GGR inayosimamiwa na Mama Sarah Masasi leo wamefanya kikao cha ushirikiano baina ya pande mbili kwa lengo la kukuza uwekezaji na kukuza biashara ya Dhahabu nchini.

Kikao hicho ambacho kimehudhuriwa na mawaziri na wataalamu wa sekta mbalimbali  kimeongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Mh. Prof. Kitila Mkumbo ambapo ametumia fursa hiyo kuishukuru WGC kwa utayari wa kufanya kazi na Tanzania na kukaribisha uwekezaji mkubwa zaidi kwenye kuongeza thamani madini yetu nchini Tanzania.

Akitoa maelezo yake,Mtendaji Mkuu wa WGC  Ndg. David Tait  amesema Tanzania inafanya vizuri kushirikiana na wachimbaji wadogo na kwamba WGC wapo tayari katika kushiriki kuwajengea uwezo wachimbaji wadogo kwenye mnyororo mzima wa uzalishaji wa dhahabu pamoja na upatikanaji wa soko la uhakika la madini kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa na Baraza.

Aidha, Ndg. Pait amefurahishwa na mpango wa serikali wa utafiti wa madini na kuahidi kushirikiana na serikali katika kurusha satelaiti ili kuongeza eneo kubwa lililofanyiwa utafiti wa kina na kuwaongoza vizuri wachimbaji nchini.

Akizungumza katika mkutano huo Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde amesema mpango wa kuwawezesha wachimbaji wadogo utaleta tija na manufaa makubwa kwa kuwa kwa hivi sasa mchango wao katika kukuza uchumi kupitia madini umeongezeka sana.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Waziri wa Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana Mh. Joel Nanauka na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Doroth Gwajima wamesema mpango huu wa kuwawezesha wachimbaji wadogo wanawake na vijana kwenye mnyororo mzima wa uzalishaji wa dhahabu nchini utaleta manufaa makubwa kwa makundi hayo na kuongeza nafasi za ajira na kukuza uchumi wa wachimbaji.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals