[Latest News]: Madini ya Spinel Yapeleka Utalii wa Madini Mahenge

Tarehe : Nov. 10, 2025, 3:15 p.m.
left

 Mahenge, Morogoro

Mahenge, eneo lililopo mkoani Morogoro, Wilaya ya Ulanga limeendelea kujipatia umaarufu mkubwa duniani kutokana na madini adimu ya vito  aina  spineli, hali ambayo sasa inaliweka eneo hilo katika ramani ya utalii wa madini nchini Tanzania.

Hayo yalibainishwa  Novemba 10,2025 na Mhandisi Penina Mtego ambaye ni  msimamizi mgodi wa Ruby International  unaosimamia uchimbaji wa madini ya spineli katika kijiji cha Epanko.

Mhandisi Penina alielezea sababu iliyopelekea  kuanzishwa kwa kituo cha Utalii wa madini ya Spineli ni kutokana na ubora wa madini hayo  ambapo yanapelekea kuonekana kama  yanatengenezwa  maabara jambo linalopelekea wafanyabiashara wa  madini ya vito kimataifa, watafiti na wadau mbalimbali  kufika mahenge ili kujionea sehemu halisi yanapochimbwa madini hayo ikiwa pamoja na kutembelea sehemu maalum yanapohifadhiwa.

Mhandisi Penina alifafanua kuwa, madini ya spineli kutoka Mahenge yanajulikana kwa uzuri wake wa kipekee, hususan rangi yake ya waridi na nyekundu inayong’aa, ambayo inavutia wanunuzi na wachimbaji wa vito kutoka mataifa mbalimbali.

Aliongeza kuwa, Spineli ya Mahenge imekuwa ikitajwa mara kwa mara katika maonyesho ya vito ya kimataifa kama Tucson Gem Show nchini Marekani , Hong Kong Jewellery Fair na BangKok Thailand ikiifanya Tanzania kuwa miongoni mwa vyanzo muhimu vya madini bora duniani.

Naye, Salehe Mbura anayesimamia kitengo cha  uzalishaji katika mgodi huo alisema kuwa, uwepo wa madini hayo umekuwa chachu ya kuibuka kwa aina mpya ya utalii unaoitwa utalii wa madini, ambapo wageni hutembelea migodi, kujifunza kuhusu malezi ya madini, na kushuhudia shughuli za uchimbaji wa kiasili. Wengine huja kwa ajili ya biashara, utafiti, au kutembelea maeneo ya kihistoria yanayohusiana na uchimbaji wa madini hayo.

Mbura aliongeza kuwa, pamoja na kuvutia wageni, utalii wa madini Mahenge umechangia kukuza uchumi wa eneo hilo kwa kuleta fursa mpya za ajira katika sekta za malazi, usafiri, uuzaji wa vito, na utamaduni. Wakazi wa vijiji jirani wamenufaika kupitia mauzo ya bidhaa za ndani na huduma kwa wageni.

Kwa upande wake Mhandisi Migodi kutoka Ofisi ya Madini Mkazi, Mkoa wa Kimadini Mahenge Mhandisi Joseph Ng'itu alieleza kuwa, madini ya spinel yamekuwa si tu hazina ya thamani kwa Tanzania, bali pia daraja la kuunganisha uchimbaji, biashara, elimu na utalii. Kwa usimamizi endelevu, Mahenge inaweza kuwa kitovu cha utalii wa madini barani Afrika, ikichangia maendeleo ya kijamii na kiuchumi. 

Aidha,  aliongeza kuwa, katika kituo hicho  eneo lingine  linajumuisha makumbusho ya madini, maonesho ya vito, na mafunzo kwa wachimbaji wadogo.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals